CHINA YAKATAA KUTOA DATA ZA COVID - 19 KWA SHIRIKA LA AFYA ULIMWENGUNI ‘WHO’


 China imekataa kutoa data muhimu kwa timu ya Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) inayochunguza asili ya Covid-19, mmoja wa wanachama wake amesema hatu hiyo ni utaratibu wa kawaida.

Dk. Dominic Dwyer ameviambia vyombo vya habari kuwa timu hiyo iliomba data ya mgonjwa mpya kutoka kwa wagonjwa wa awali, kile alichokiita “mazoezi ya kawaida”.

Amesema hata hivyo walipokea muhtasari tu. Bado China haijajibu madai hayo lakini hapo awali imesisitiza ilikuwa wazi kwa WHO.

Marekani imeitaka China kutoa data zinazopatikana kutoka katika hatua za mwanzo za mlipuko, ikisema ina “wasiwasi mkubwa” kuhusu ripoti ya WHO.

Wiki iliyopita, timu ya WHO ilihitimisha kwamba “haiwezekani kabisa” kwamba virusi vya corona vilivuja kutoka kwenye maabara katika mji wa Wuhan, ikiondoa nadharia yenye utata iliyoibuka mwaka jana.

Wuhan ilikuwa mahali pa kwanza ulimwenguni ambapo virusi hivyo viligunduliwa, mwishoni mwa 2019.

Tangu wakati huo, zaidi ya watu milioni 106 walipata maambukizi na vifo vya watu milioni 2.3 vimeripotiwa ulimwenguni.

-BBC



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments