BABA MZAZI WA NICKI MINAJ AFARIKI DUNIA

Onika Tanya Miraj maarufu Nicki Minaj

Baba wa mwanamuziki wa miondoko ya kufokafoka, Nicki Minaj, 64, ameaga dunia baada ya kugongwa na gari kisha dereva kukimbia mjini New York, polisi wameeleza.


Robert Miraj alikuwa akitembea kando kando ya barabara katika kisiwa cha Long siku ya Ijumaa na kugongwa na gari, kisha dereva wa gari hiyo aliendelea na safari, polisi katika kaunti ya Nassau imesema.

Miraj alipelekwa hospitalini ambako alithibitishwa kufariki siku ya Jumamosi.

Polisi wametaka shuhuda yeyote wa tukio hilo baya kujitokeza. Gazeti la the Guardian limeripoti .

Minaj, 38, kwa jina Onika Tanya Miraj alizaliwa huko Trinidad na alikulia jijini New York City borough of Queens.

Mwanamuziki huyo hajajitokeza kuzungumza chochote kuhusu kifo cha baba yake.

Chanzo- BBC SWAHILI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post