TCRA YASITISHA UTOAJI WA LESENI ZA MAUDHUI MTANDAONI

Mkuu wa TCRA Kanda ya Ziwa, Mhandisi Mihayo akizungumza kwenye Usiku wa Waandishi wa Habari na Wadau wa Habari Kanda ya Ziwa katika ukumbi wa Gold Crest Hotel Jijini Mwanza.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mamlaka ya Mawasiliano ya Tanzania (TCRA) imetangaza kusitisha utoaji wa leseni za Maudhui Mtandaoni kwa muda kuanzia Januari 28,2021 hadi Juni 30,2021.

Akizungumza leo Jumatatu Februari 1,2021 kwenye Usiku wa Waandishi wa Habari na Wadau wa Habari Kanda ya Ziwa katika ukumbi wa Gold Crest Hotel Jijini Mwanza, Mkuu wa TCRA Kanda ya Ziwa, Mhandisi Mihayo amesema hatua ya kusitisha utoaji leseni kwa Blogs na Online Tv inatokana na kuendelea kuwepo kwa ukiukwaji mkubwa wa matumizi sahihi ya mtandao.

“Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuanzia tarehe 28 Januari, 2021 imesitisha utoaji leseni za maudhui mtandaoni kwa muda hadi tarehe 30 Juni 2021 ili kutoa fursa kwa TCRA kufanya tathmini na kuja na hatua muhimu za kurekebisha dosari nyingi zilizojitokeza”,amesema Mhandisi Mihayo.

Mhandisi Mihayo pia amewataka watoa huduma wa sekta ya utangazaji kutekeleza matakwa ya kanuni ya uendeshaji ikiwemo kuwalipa mishahara watumishi wao.

Aidha amewasihi waandishi wa habari kupendana na kushirikiana na kuhakikisha wanajiendeleza kielimu  kuanzia ngazi ya Diploma ili kukidhi vigezo vinavyotakiwa.

Mkuu wa TCRA Kanda ya Ziwa, Mhandisi Mihayo akizungumza kwenye Usiku wa Waandishi wa Habari na Wadau wa Habari Kanda ya Ziwa katika ukumbi wa Gold Crest Hotel Jijini Mwanza. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa TCRA Kanda ya Ziwa, Mhandisi Mihayo akizungumza kwenye Usiku wa Waandishi wa Habari na Wadau wa Habari Kanda ya Ziwa katika ukumbi wa Gold Crest Hotel Jijini Mwanza.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments