Tanzia : MHASIBU WA MANISPAA YA SHINYANGA SEIF HAMAD MANDE AFARIKI DUNIA


Seif Hamad enzi za uhai wake
Mhasibu wa Manispaa ya Shinyanga Seif Hamad Mande amefariki dunia leo jioni Alhamisi 18,2021 wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

Meya wa Manispaa ya Shinyanga David Nkulila amethibitisha taarifa za kifo cha Seif Hamad Mande akieleza kuwa alikuwa ameugua kwa muda mrefu.

Seif Hamad Mande amewahi kuwa Mweka Hazina wa timu ya Stand United na amekuwa Mjumbe wa Bodi ya Shirika la Rafiki SDO linalojihusisha na utetezi wa haki za wanawake na watoto na masuala mbalimbali ya kijamiiMungu ailaze Mahali pema peponi roho ya marehemu Seif Hamad Mande. Amina.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post