MAALIM SEIF AZIKWA KIJIJINI KWAO MTAMBWE - PEMBA | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, February 18, 2021

MAALIM SEIF AZIKWA KIJIJINI KWAO MTAMBWE - PEMBA

  Malunde       Thursday, February 18, 2021

Mwili wa Maalim Seif Sharif Hamad, ukiwekwa kwenye nyumba yake ya milele
**
Safari ya maisha ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad, imefikia mwisho jioni ya leo, mara baada ya mwili wake kupumzishwa katika nyumba yake ya milele kijijini kwake Mtambwe, visiwani Pemba.

Mapema leo asubuhi mwili wa Maalim Seif, uliswaliwa katika msikiti wa Maamur Upanga jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, na kisha baadaye ulisafirishwa hadi Zanzibar na kupelekwa katika viwanja vya Mnazi Mmoja kwa ajili ya Dua maalum.

Mazishi ya Maalim Seif, yameongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ya Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi, pamoja na viongozi wengine mbalimbali wa serikali na wa vyama kutoka vyama mbalimbali vya kisiasa nchini.

Maalim Seif alifariki dunia Februari 17, 2021, katika hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa anapatiwa matibabu.

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post