Tanzia : ALIYEKUWA GAVANA WA BENKI KUU YA TANZANIA PROF. BENNO NDULLU AFARIKI DUNIA | MALUNDE 1 BLOG

Monday, February 22, 2021

Tanzia : ALIYEKUWA GAVANA WA BENKI KUU YA TANZANIA PROF. BENNO NDULLU AFARIKI DUNIA

  Malunde       Monday, February 22, 2021

Profesa Benno Ndullu enzi za uhai wake
***
Aliyewahi kuwa Gavana Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndullu (71) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Februari 22,2021 katika hospitali ya Hubert Kairuki Memorial University alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Katibu muhtasi wake, Msafiri Nampesya ameithibitisha kuhusu kifo hicho.

Profesa Ndullu alikuwa Gavana wa Benki kuu ya Tanzania, kuanzia 2008 hadi 2018 na pia aliwahi kuwa Mhadhiri wa Uchumi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kwamba aliwahi kufanya kazi Benki ya Dunia.

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post