Tanzia : MBUNGE ATASHASHTA NDITIYE AFARIKI DUNIA


Mbunge wa Muhambwe mkoani Kigoma na ambaye pia alikuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Mhandisi Atashasta Justus Nditiye amefariki dunia leo Ijumaa Februari 12,2021 saa 4:00 asubuhi.

Spika wa Bunge Job Ndugai amethibitisha habari hizo akisema Nditiye alifariki wakati akipatiwa matibabu baada ya ajali ya gari aliyopata Februari 10, 2021 eneo la Nanenane Nzuguni mkoani Dodoma.

Kutokana na kifo hicho, Ndugai ameahirisha shughuli za Bunge hadi kesho Jumamosi wakati patakapotolewa taarifa za taratibu za kuaga mwili na maziko.

Nditiye anakuwa mbunge wa pili kufariki dunia katika Bunge la 12 baada ya Martha Umbulla, aliyekuwa mbunge wa viti maalum (CCM), kufariki hivi karibuni.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post