RAIS WA ZANZIBAR AUNGANA NA WANANCHI KUUSWALIA MWILI WA MAALIM SEIF SHARIF HAMAD VIWANJA VYA MNAZI MMOJA ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi na Viongozi wengi wakijumuika na Wananchi wa Zanzibar katika Sala ya kuusalia mwili wa marehemu aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, iliyoongozwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi, iliyofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Zanzibar leo 18-2-2021. Picha na Ikulu

Makanali na Mameja wa JWTZ wakiwa wamebeka jeneza la Mwili wa aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad uliopowasiliu Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, kwa ajili ya kuagwa na Wananchi wa Zanzibar katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi akiwa na Viongozi wakiaga baada ya kumalizika kwa Sala ya kumuombea aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, iliyofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi na Viongozi wa Dini na Serikali wakiitikia dua ikisomwa na Katibu wa Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Abdalla Talib, baada ya kumalizika kwa Sala ya kuusalia mwili wa aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, iliofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Zanzibar.
Baadhi ya wananchi wakiwa katika mazishi ya MaalimSeif (Picha na Ikulu)

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments