Tanzia : ERASTO IZENGO KWILASA AFARIKI DUNIA

Erasto Kwilasa enzi za uhai wake
Erasto Kwilasa enzi za uhai wake
Julai 20, 2020 Erasto Kwilasa akiomba kura achaguliwe kuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia CCM.

***
Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Shinyanga Erasto Izengo Kwilasa mwaka 2016 hadi 2017 amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Ijumaa Februari 5,2021.

Erasto Izengo Kwilasa ambaye alikuwa miongoni mwa watia nia 60 kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia CCM katika uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2020 amefariki dunia wakati akiendelea kupatiwa matibabu Nairobi nchini Kenya.

Akizungumza na Malunde 1 blog, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Mabala Mlolwa amethibitisha taarifa za kifo cha Mzee Erasto Kwilasa ambaye pia alikuwa anajishughulisha na kazi za Ukandarasi.

“Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha ndugu yetu, mpendwa wetu Erasto Kwilasa. Taarifa nilizopewa ni kwamba amefariki dunia akiwa nje ya nchi. Tutaendelea kupeana taarifa zaidi”,amesema Mabala.

Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu Erasto Kwilasa. Amina.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post