Picha : WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AONGOZA MAZISHI YA BALOZI KIJAZI

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa leo tarehe 20 Februari, 2021 ameongoza mamia ya waombolezaji kwenye maziko ya aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Mhandisi John William Kijazi yaliyofanyika kwenye makaburi yaliyoko katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mt. Augustino Manundu Korogwe, Tanga.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka Shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi katika mazishi yaliyofanyika kwenye Makaburi ya Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Augustino lililopo eneo la Manundu Korogwe, Februari 20, 2021. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitupa udongo kwenye kaburi la aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi katika Mazishi yaliyofanyika kwenye Makaburi ya Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Augustino eneo la Manundu Korogwe, Februari 20, 2021. Kushoto ni Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole, Francisca Kijazi, Mjane wa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi , Balozi John Kijazi katika Ibada ya kumwombea marehemu iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Augustino lililopo Manundu Korogwe, Februari 20, 2021.
Mawaziri wakiweka shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi katika mazishi yaliyofanyika kwenye Makaburi ya Kanisa Katoliki la Mtakatifu Augustino, eneo la Manundu Korogwe, Februari 20, 2021. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alimwakilisa Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika mazishi hayo. Kutoka kushoto ni , Dkt. Dorothy Gwajima, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Juma Aweso, Waziri wa Maji, Ummy Mwalimu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayesugulikia Muungano na Mazingira, Profesa Joyce Ndalicako, Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia na kulia ni Jenista Mhagama, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments