MBUNGE KATAMBI ATOA BIMA ZA AFYA KWA WATOTO 272 WENYE MAHITAJI MAALUMU ...DIWANI AANDAA CHAKULA CHA PAMOJA NA WATOTO NA WANANCHI

Katibu wa Siasa na Uenezi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Saidi Ahmed Bwanga akiwa ameshikilia bima za afya za ajili ya watoto 172 wenye mahitaji maalumu katika Manispaa ya Shinyanga zilizotolewa na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Diwani wa Kata ya Ibinzamata Manispaa ya Shinyanga Mhe. Ezekiel John Sabo amefanya hafla ya kula chakula cha pamoja na watoto wenye mahitaji maalumu na wananchi wote wa kata ya Ibinzamata ikiwa ni sehemu ya kuwashukuru wananchi kwa kumchagua kuwa diwani katika uchaguzi Mkuu mwaka 2020.

Hafla hiyo iliyofanyika Jumapili Februari 7,2021 imeenda sambamba na maadhimisho ya miaka 44 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kata ya Ibinzamata ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu wa Siasa na Uenezi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Saidi Ahmed Bwanga.

Sabo amesema ameamua kula chakula cha pamoja na watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija ili kuwaonesha upendo watoto hao lakini kula chakula na wananchi wa kata ya Ibinzamata ili kuwashukuru kwa kumchagua kuwa diwani wao na kuchagua mbunge Patrobas Katambi na Rais John Pombe Magufuli katika uchaguzi mkuu 2020.

“Ninakipongeza Chama cha Mapinduzi kwa ushindi mnono katika uchaguzi mkuu 2020.Nawashukuru na kuwapongeza walimu na walezi wa watoto wenye mahitaji maalumu jinsi wanavyojitolea kuhudumia watoto hawa vizuri”,amesema Sabo.

Akizungumza katika sherehe hizo, Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Said Bwanga amemshukuru na kumpongeza Diwani wa kata ya Ibinzamata  Ezekiel John Sabo kwa kuandaa sherehe hizo na kueleza kuwa CCM kudumisha amani na ushirikiano.

“Tunaposherehekea miaka 44 ya CCM tuna kila sababu ya kutembea kifua mbele kujivunia mafanikio tuliyofikia. Tunaendelea kujivunia amani na upendo hivyo tuwaepuke baadhi ya watu wanaotumiwa na Mabeberu kuharibu sifa ya nchi yetu”,amesema Bwanga.

Katika hatua nyingine amewataka Madiwani, Maafisa Watendaji na baadhi ya viongozi wanaolazimisha wananchi kuchangia ujenzi wa shule, madarasa na madawati kwa lazima na walimu kutowarudisha nyumbani wanafunzi ambao hawajatoa michango bali wananchi wanatakiwa kuelimishwa ili wachangie kwa hiari.

Katika sherehe hizo, Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Mhe. Patrobas Katambi ametoa msaada wa Bima za Afya za CHF iliyoboreshwa kwa watoto 272 wenye uhitaji maalumu kutoka vituo vitatu ambavyo ni Buhangija kinacholea watoto wenye ualbino,wasioona na Viziwi 231, kituo cha watoto wenye utindio wa ubongo cha Kitangiri watoto 21 na kituo cha Bushushu kata ya Lubaga watoto 20.

Bima hizo za afya kwa ajili ya watoto wenye mahitaji maalumu zimekabidhiwa na Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Samwel Jackson akimwakilisha Mbunge Patrobas Katambi ambaye yupo Jijini Dodoma akiendelea na majukumu mengine.

Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya Gilitu Enterprises Ltd Gilitu Nilla Makula ametoa msaada wa Televisheni (Flat Screen) na Dish Dish la Azam katika kituo cha kulelea watoto cha Buhangija kwa ajili ya kuangalia taarifa mbalimbali.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Katibu wa Siasa na Uenezi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Saidi Ahmed Bwanga akizungumza wa hafla ya Diwani wa Kata ya Ibinzamata Ezekiel John Sabo kula chakula cha pamoja wananchi na watoto wenye mahitaji maalumu katika Kituo cha Buhangija kilichopo katika kata ya Ibinzamata sambamba na maadhimisho ya Miaka 44 ya Chama Cha Mapinduzi Jumapili Februari 7,2021. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Katibu wa Siasa na Uenezi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Saidi Ahmed Bwanga akizungumza wa hafla ya Diwani wa Kata ya Ibinzamata Ezekiel John Sabo kula chakula cha pamoja wananchi na watoto wenye mahitaji maalumu katika Kituo cha Buhangija kilichopo katika kata ya Ibinzamata sambamba na maadhimisho ya Miaka 44 ya Chama Cha Mapinduzi Jumapili Februari 7,2021.
Diwani wa Kata ya Ibinzamata Ezekiel John Sabo akizungumza wakati wa hafla aliyoiandaa kwa ajili ya kula chakula cha pamoja wananchi na watoto wenye mahitaji maalumu katika Kituo cha Buhangija kilichopo katika kata ya Ibinzamata sambamba na maadhimisho ya Miaka 44 ya Chama Cha Mapinduzi Jumapili Februari 7,2021.

Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Samwel Jackson akielezea kuhusu Bima za Afya za CHF iliyoboreshwa zilitolewa na Mbunge Patrobas Katambi kwa watoto 272 wenye uhitaji maalumu kutoka vituo vitatu ambavyo ni Buhangija kinacholea watoto wenye ualbino,wasioona na Viziwi 231, kituo cha watoto wenye utindio wa ubongo cha Kitangiri watoto 21 na kituo cha Bushushu kata ya Lubaga watoto 20.
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Mhe. Patrobas Katambi, Bw. Samwel Jackson akionesha Bima za Afya za CHF iliyoboreshwa kwa watoto 272 wenye uhitaji maalumu zilizotolewa na Mbunge Patrobas Katambi.
Sehemu ya Bima za Afya za CHF iliyoboreshwa kwa watoto 272 wenye uhitaji maalumu zilizotolewa na Mbunge Patrobas Katambi.
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Mhe. Patrobas Katambi, Bw. Samwel Jackson akimkabidhi Katibu wa Siasa na Uenezi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Saidi Bwanga (kulia) Bima za Afya za CHF iliyoboreshwa kwa watoto 272 wenye uhitaji maalumu zilizotolewa na Mbunge Patrobas Katambi.

Katibu wa Siasa na Uenezi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Saidi Ahmed Bwanga akiwakabidhi watoto bima za afya ambazo ni sehemu ya kadi za bima ya afya kwa ajili ya watoto 272 wenye mahitaji maalumu katika Manispaa ya Shinyanga zilizotolewa na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi.
Katibu wa Siasa na Uenezi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Saidi Ahmed Bwanga akimkabidhi mtoto bima ya afya ambayo ni sehemu ya kadi za bima ya afya kwa ajili ya watoto 272 wenye mahitaji maalumu katika Manispaa ya Shinyanga zilizotolewa na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Gilitu Enterprises Ltd Gilitu Nilla Makula akizungumza wakati wa sherehe hizo ambapo ametoa msaada wa Televisheni (Flat Screen) na Dish Dish la Azam katika kituo cha kulelea watoto cha Buhangija kwa ajili ya kuangalia taarifa mbalimbali.
Mwenyekiti wa kamati ya chakula kwenye hafla ya chakula pamoja maadhimisho ya miaka 44 ya CCM, Teddy Shaban ambaye alikuwa Meneja Kampeni wa Diwani Ezekiel John Sabo akizungumza wakati hafla hiyo.
Afisa Mtendaji wa kata ya Ibinzamata Victor Kajuna akizungumza kwenye hafla hiyo.
Viongozi mbalimbali wakiwa meza kuu.
Viongozi mbalimbali wakiwa meza kuu
Viongozi mbalimbali wakiwa meza kuu
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Dotto Joshua akizungumza wakati wa sherehe hizo
Katibu wa UVCCM mkoa wa Shinyanga, Muhsin Zikatim akizungumza kwenye sherehe hizo

Kaimu Katibu CCM Kata ya Ibinzamata ambaye ni Katibu wa Siasa na Uenezi kata ya Ibinzamata Ibrahim Abdallah akizungumza wakati wa sherehe hizo

Mwenyekiti wa CCM kata ya Ibinzamata, Haruna Seleman Mkuki akizungumza kwenye sherehe hizo
Watoto wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea
Watoto wakiwa eneo la tukio
Watoto wakiwa katika eneo la tukio
Sherehe zikiendelea

Sherehe zikiendelea
Sherehe zikiendelea
Mabago Ibrahim akisoma risala kwa niaba ya Katibu wa CCM kata ya Ibinzamata
Wananchi na wachama wa CCM wakiwa kwenye sherehe

Kamati ya chakula wakijiandaa kugawa chakula kwa watoto na wananchi wa kata ya Ibinzamata.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments