ATOKWA JASHO JEMBAMBA BAADA YA KUFUMANIWA AKIPAKUA ASALI YA MKE WA MWANAJESHI LIVE KITANDANIJamaa mmoja kutoka mtaani Kawangware, Nairobi nchini Kenya ametokwa na kijasho chembamba baada ya kunaswa akitafuna asali ya wenyewe na kisha kupewa sharti lililomvunja moyo.

 Inasemekana mwenye nyumba ambaye ni Mwanajeshi alimwambia kwa hasira kwamba naye angeenda kwake kulipiza kisasi kwa kuchovya asali ya mrembo wake hadi asubuhi.

“Kwa kuwa unajiona kidume cha mwanaume kurina asali yangu,ni zamu yangu kwenda kwa mkeo nikakeshe naye. Hautoki humu maana nawafungia kwa kufuli mbili,” mwenye nyumba alisema kwa dharau.

 Kulingana na Taifa Leo, kabla ya kijogoo kunaswa hatimaye, inasemekana alikuwa amemnyemelea mke wa jamaa huyo kwa muda mrefu. 

“Mzinga wako unarambwa kurambwa na huna habari?” jirani alimpasha jamaa.

“Nani anacheza na kifo? Nani huyo asiyethamini maisha yake?” jamaa aliuliza. “Weka mtego usiku huu na unamjua. Lipo dume linalounguruma kwako pindi ukiondoka,” jirani aliongeza.

 Penyenye zinaarifu kwamba jamaa alirejea nyumbani usiku huo na kumkuta dume alililolifahamu vyema limempakata mkewe kitandani.

 “Humu ndani mna chakula cha kutosha. Usiwe na haraka kutoka. Leo naenda kunguruma kwako,” jamaa aliwaka huku akifunga mlango kwa nje.

 Duru zinasema kwamba kijogoo alishtuka sana na kumuomba jamaa wazungumze.

 “Hakuna cha kuzungumza. Mkuki kwa nguruwe mtamu,kwa binadamu mchungu.” “Sasa meza ukweli wako hata ingawa unauma!” jamaa alinguruma na kuwaacha wawili hao wakikuna vichwa.

 Hata hivyo, haikufahamika iwapo ni kweli jamaa alielekea kwa mke wa kijogoo.

 Semasema kijogoo alipohisi mambo yamekuwa mabaya alivunja dirisha na kutoroka kuelekea kwake, naye mke wa afande akamfuata akihofia mumewe angemtwanga akirudi.

Chanzo - Tuko News

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post