MCHUNGAJI WA KANISA AGOMA KUPELEKA WATOTO SHULE AKIDAI NI DHAMBI


Merchades Buberwa, Baba wa familia

Familia ya Merchades Buberwa, mkazi wa Kasarani, Bukoba mkoani Kagera, imeeleza haina mpango wa kuwapeleka shule, lakini pia watu wa familia hiyo hawamiliki simu, hawaangalii televisheni na hawashiriki shughuli zozote za kijamii wakidai kuwa Mungu wao anakataza na kufanya hivyo ni dhambi.

Hayo yote yanajiri baada ya Mkuu wa wilaya ya Bukoba Deodatus Kinawiro, kumwagiza afisa elimu ya msingi wa manispaa hiyo, kuwakamata na kuwapeleka shuleni kwa nguvu, watoto watatu wa familia hiyo ya anayejiita mchungaji aliyekataa kuwapeleka watoto wake shule kwa madai ya kuwa kufanya hivyo ni dhambi maana maandiko ya Mungu hayaruhusu watoto kwenda shule.

Familia hiyo inao watoto watano na wote hawasomi na mkubwa kati yao ni wa kike mwenye umri wa miaka 13, mbali na kutokwenda shule, wakiwa wadogo hawajawahi kupelekwa kliniki na pia wakiumwa hawapelekwi hospitali, ambapo mkuu huyo wa wilaya amesema baba huyo akiendelea kushikilia msimamo wake wa kuzuia watoto kwenda shule atakamatwa na kushtakiwa.

Baba wa watoto hao Merchades Buberwa ambaye amesema ni mchungaji wa kanisa la Wakristo washikao amri za Mungu, ambalo makao yake makuu yako mbinguni, amesema hayuko tayari kuruhusu watoto wake kutenda dhambi kwa kwenda shule, huku mkewe Agripina Maganja, akimweleza mkuu huyo wa wilaya kuwa Mungu atasimama kuwatetea.

Via>> EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments