TRAFIKI AKAMATWA KWA KUOMBA RUSHWA YA NGONO AKAMILISHE UCHUNGUZI | MALUNDE 1 BLOG

Friday, January 8, 2021

TRAFIKI AKAMATWA KWA KUOMBA RUSHWA YA NGONO AKAMILISHE UCHUNGUZI

  Malunde       Friday, January 8, 2021


Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kilimanjaro inamshikilia Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Peter Albert Moshi kwa tuhuma za kuomba Rushwa ya Ngono.

Askari huyo alikuwa akichunguza ajali ya pikipiki ambayo ilimgonga mtoto na kusababisha kuvunjika mkono. Aliomba Rushwa Ngono kwa mama wa mtoto ili aweze kukamilisha Taarifa za Uchunguzi.

Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Kilimanjaro, Frida Wikesi amesema, askari huyo amekamatwa Januari 6 akiwa nyumba ya kulala wageni maeneo ya Soweto Mjini Moshi.

Uchunguzi wa TAKUKURU umebaini kuwa, Peter alimsumbua mama wa mtoto kwa muda mrefu na hivyo kusababisha shauri kuchelewa hali iliyopelekea mama huyo kupeleka malalamiko na wakaweka mtego wa kumkamata.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post