ASKARI POLISI WANNE WASIMAMISHWA KAZI KWA UTOVU WA NIDHAMU


Na Woinde Shizza ,ARUSHA
Jeshi la Polisi nchini limewafukuza kazi kwa fedheha askari wake wanne kutokana na makosa mbalimbali ya utovu wa nidhamu ,rushwa na wizi.

Akiongea na vyombo vya habari Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha ,Salumu Hamduni alisema kuwa askari hao wametimuliwa kazi jana januari 6,Mwaka huu .


Alisema kabla ya kufukuzwa  kazi kwa askari hao ,walifikishwa kwenye mahakama ya kijeshi na kukutwa na hatia na kwamba watafikishwa mahakamani Kama vibaka wengine wanaojihusisha na matukio ya uhalifu


“Askari hao tumewafukuza kazi baada ya kuwafikisha kwenye mahakama ya kijeshi na watashtakiwa Kama vibaka wengine wa kawaida”alisema Kamanda


Aliwataja askari hao kuwa ni pamoja na  askari mwenye namba G. 5134 DC Heavenlight Mushi  aliyekuwa Askari kitengo Cha Intelijensia Mkoa wa kipolisi kinondoni jijini Dar es Salaam,H.125 PC Gasper Paul kitengo Cha Intelijensia makao makuu Dodoma na H.1021 PC Bryton Murumbe aliyekuwa askari wa kawaida mkoani Dodoma.


Kamanda alifafanua kwamba askari hao wamefukuzwa kazi kutokana kwa kosa la kumteka mfanyabiashara wa Madini jijini Arusha,Sammy Mollel ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya madini ya Germs and Rocks Venture ya jiji Arusha na kujipatia kiasi cha sh, milioni 10 kinyume cha sheria.


Alisema askari hao wakikamatwa desemba 24,2020 katika ofisi za mfanyabiashara huyo baada ya kufika kwa ajili ya kuchukua mgao wa pili wa shilingi milioni 20 kati ya milioni 30 walizohitaji na kupatiwa sh,milioni 10.


Mwingine aliyefukuzwa kazi ni askari mwenye namba F.1445 CPL Koplo William Joseph mkazi wa Muriet jiji Arusha ambaye alikamatwa jana nyumbani kwake akiwa na na bidhaa mbalimbali haramu ikiwemo misokoto ya bangi.


Alisema kuwa askari huyo alikutwa na misokoto 20 ya bangi bhangi kwenye gari lake ,kukiunganishia umeme wa wizi kinyume cha sheria,kupatikana na pombe ya gongo lita tano na lita mafuta ya Dizel Lita 85.


Pia alikutwa na vyuma vya bomba kinyume na taratibu,pombe ya viroba boksi 84 iliyookatazwa na serikali,chupa 9 za konyagi na pakti 3 za pombe aina ya kiroba .


Kamanda alisema kuwa upelelezi wa matukio hayo umekamilika na majalada yamepelekwa ofisi ya taifa ya mashtaka kwa ajili ya hatua zaidi na majalada hayo yakirudi watafikishwa mahakamani.




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments