MAYALA : WAFUGAJI WA KUKU MJIKITE ZAIDI KATIKA KUMKINGA KUKU DHIDI YA MAGONJWA BADALA YA TIBA

Mtaalamu wa Magonjwa ya Kuku kutoka Silver Land Tanzania Bw. Daudi Mayala
Na Josephine Charles - Shinyanga
Rai imetolewa kwa wafugaji wa kuku kujikita zaidi katika kumkinga kuku dhidi ya magonjwa na siyo tiba.

Rai hiyo imetolewa na Mtaalamu wa Magonjwa ya kuku kutoka Silver Land Tanzania Bw. Daudi Mayala wakati akizungumza Katika Kipindi cha Mambo Leo kinachorushwa na Radio Faraja fm stereo kila Juma tatu hadi Ijumaa saa tatu asubuhi hadi saa saba kamili mchana. 

Amesema wafugaji wengi wa kuku hawana tabia ya kumkinga kuku dhidi ya magonjwa badala yake wan kuwa wa kwanza kumwambukiza kuku magonjwa pasipo wao kujua kwa kutokuzingatia mavazi na usafi wakati wa kuingia kwenye vibanda vya kuku hivyo hujikuta wamewapelekea kuku virusi vinavyosababisha ugonjwa kwa kuku na ndipo huanza kuhangaika kutafuta dawa za kutibu ule ugonjwa matokeo yake huchelewa na kusababisha kuku kufa. 

Ameyataja baadhi ya magonjwa ambayo huwapata kuku mara kwa mara kuwa ni Kideri,Gumboro,Ndui,Koraiza,Typhoid,TB na ugonjwa wa mfumo wa upumuaji ambapo baadhi ya hayo magonjwa mengine huwapata kuku kwa njia ya Virusi na Bakteria.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post