AKAMATWA UWANJA WA NDEGE AKISAFIRISHA VINYONGA 74 | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, January 26, 2021

AKAMATWA UWANJA WA NDEGE AKISAFIRISHA VINYONGA 74

  Malunde       Tuesday, January 26, 2021


Mwanaume mwenye umri wa miaka 56 ambaye hakutambuliwa zaidi  amekamatwa na Mamlaka nchini Austria katika uwanja wa ndege wa Vienna akiwa anatorosha vinyonga 74 kutoka nchini Tanzania.

Kwa Mujibu  wa gazeti la The Telegraph la Uingereza jamaa huyo alikuwa amewaficha wanyama hao katika soksi na masanduku ya barafu alipokamatwa na maofisa forodha wa uwanja huo wa Vienna.

Naibu katibu mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii nchini Tanzania, Allan Kijazi amesema mwanaume huyo alisafiri kwenda Austria kutoka Tanzania kupitia Ethiopia na kwamba mujibu wa gazeti hilo vinyonga hao walikuwa wakipelekwa kwenye bustani ya wanyama ya Schoenbrunn na ilibainika kuwa watatu wamekufa.

Amesema wanyama wote walikuwa wanatoka katika milima ya Usambara Tanzania na walikuwa katika umri wa wiki moja hadi wakubwa ambao walitakiwa kuuzwa katika masoko ya ulanguzi.



Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post