JESHI LA POLISI SHINYANGA LAKANUSHA TAARIFA ZA DEREVA WA LORI ALIYEPIGWA NA ABIRIA WA BASI LA FRESTER KUFARIKI DUNIA

 
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba
***

Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limekanusha taarifa zinazoenea mtandaoni kuwa dereva wa lori aliyeshambuliwa kwa kupigwa ngumi na mateke na abiria wa Basi la Frester kwa madai ya kutaka kusababisha ajali, amefariki dunia baada ya kuwa chini ya uangalizi wa madaktari hospitali alikokuwa amelazwa kwamba aliumia kwa ndani.

Akizungumza na Malunde 1 blog leo Januari 2,2021 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba amesema taarifa za kwamba dereva huyo amefariki dunia ni za uongo na kuwataka wananchi kutumia vizuri mitandao ya kijamii kwani ni kosa kisheria kueneza taarifa za uongo.

"Baada ya Jeshi la polisi kuona taarifa hizo mtandaoni tumefuatilia na kubaini ni uzushi tu. Ni taarifa ya uongo, nimempigia simu huyo dereva, Emmanuel Norbert Msuya aliyeshambuliwa, yupo salama anaendelea na majukumu yake ya kila siku",amesema Kamanda Magiligimba.
Dereva wa Lori Emmanuel Nobert Msuya (30) mwenye shati la bluu akishambuliwa kwa ngumi na mateke na abiria wa basi la Frester wakimtuhumu kutaka kusababisha ajali eneo la Samuye barabara ya Shinyanga - Mwanza Desemba 21,2020 majira ya saa 11 jioni katika kijiji cha Samuye,kata ya Samuye wilaya ya Shinyanga.

 Soma pia:



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments