KATAMBI ARIDHISHWA KASI UJENZI VYUMBA VYA MADARASA, AMWAGA MAMILIONI YA FEDHA

 

 Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi, (katikati) ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, akishiriki kwenye ujenzi wa vyumba vya Madarasa katika shule ya Msingi Mlimani Old Shinyanga.


Na Marco Maduhu, Shinyanga. 
Naibu Waziri Wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira Patrobas Katambi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, ameshiriki ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule za msingi na sekondari manispaa ya Shinyanga, na kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa vyumba hivyo.


Katambi alianza ziara yake Desemba 31 mwaka 2020, na leo Januari 2, 2021 amehitimisha ziara hiyo ya kushiriki na kuhamasisha ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule za msingi na sekondari halmashauri ya manispaa ya Shinyanga na kutoa kiasi cha fedha Shilingi Milioni 34, ili kuunga mkono ujenzi wa vyumba hivyo. 

Amesema katika ziara hiyo ameridhishwa na ujenzi wa maboma ya vyumba hivyo vya madarasa ambayo yanajengwa kwa kiwango kinachotakiwa, pamoja na kasi ya kumalizia haraka wa jenzi hizo, ili wanafunzi watakapofungua shule waanze kuyatumia kusoma na kufanya vizuri kwenye masomo yao. 

“Nashukuru sana wananchi kwa kujitoa nguvu kazi na michango yenu kushiriki kuchangia shughuli za maendeleo kwenye ujenzi huu wa vyumba vya madarasa, na mimi kama mbunge wenu nimeamua kushiriki na ninyi kwenye ujenzi huu wa vyumba vya madarasa, pamoja na kutoa fedha ili tukamilishe zoezi hili haraka na wanafunzi wasome katika mazingira mazuri,” amesema Katambi. 

“Natoa wito pia kwa wadau wa elimu, zikiwemo taasisi za kifedha, makampuni, wajitokeze kuchangia ujenzi wa miundombinu ya shule ikiwamo vifaa vya maabara na madawati, ili majengo haya yatakapokamilika na vifaa hivyo viwepo na siyo wanafunzi kuanza kukaa chini sababu ya upungufu wa madawati,” ameongeza. 

Pia ameiomba halmashauri iwe inagawa idadi sawa ya walimu hasa katika shule za pembezoni mwa mji ambazo zinakabiliwa na upungufu wa walimu ikilinganishwa na idadi ya wanafunzi. 

“Mfano katika shule ya msingi Twendepamoja iliyopo Mwamalili, ina jumla ya Wanafunzi 984, lakini kuna walimu Watano tu, na mmoja nimepewa taarifa anataka kuondoka hivyo itabakiwa na walimu Wanne kwa shule nzima, hili si sawa naomba uwiano uwepo kwa shule za mjini na pembezoni mwa mji, ili watoto wetu wafundishike na kufaulu,”ameeleza Katambi. 

Katika hatua nyingine ameipongeza halmashauri ya manispaa ya Shinyanga kwa kuanzisha kiwanda chao cha ufyatuaji wa matofali, ambayo wanayatumia kwenye ujenzi wa miradi mbalimbali ya Serikali na kuokoa gharama pamoja na kujenga majengo kwa kiwango kinachotakiwa sababu ya uimara wa matofari hayo. 

Naye Mstahiki Meya wa manispaa ya Shinyanga David Nkulila, amesema kasi ambayo imeonekana kwenye ujenzi huo wa vyumba vya madarasa, ndiyo kasi ambayo wataendelea nayo kwenye utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi, ili kuendana na kasi ya Rais John Magufuli. 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi amesema Serikali inashirikiana kikamilifu na wananchi kwenye ujenzi huo wa vyumba vya madarasa, na kubainisha katika Halmshauri hiyo inaupungufu wa vyumba 100, kwa shule za Msingi upungufu wa vyumba 64 na Sekondari vyumba 34. 

Nao baadhi ya wanafunzi David Sharif anayesoma darasa la nne katika shule ya Msingi Ng’wihando, amemshukuru Mbunge Katambi kwa kushiriki kujenga vyumba hivyo vya madarasa, pamoja na Rais John Magufuli kwa kutoa elimu bila malipo ambayo imewafanya wasome ili kutumiza ndoto zao, huku akisema ndoto zake ni kuja kuwa Mbunge. 

TAZAMA PICHA HAPA CHINI 
 
Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, akielezea hitimisho la ziara yake ya ushiriki na uhamasishaji ujenzi wa vyumba vya madarasa, kushoto ni Mstahiki Meya wa manispaa ya Shinyanga David Nkulila na kushoto ni Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga David Nkulila, akizungumza kwenye hitimisho la ziara ya Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, na Ajira, Patrobas Katambi, wa kwanza kulia ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, kushoto ni Afisa elimu wa Shule za msingi manispaa ya Shinyanga Neema Mkanga.
Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi, akizungumza kwenye hitimisho la ziara ya Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini.
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini (katikati), akishiriki ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya Masingi Mlimani iliyopo Kata ya Old Shinyanga.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini akikagua ukuta wa Jengo la Shule ya Sekondari Kolandoto na kubaini kuwa umejengwa kwa kiwango kinachotakiwa.
Ukaguzi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya Sekondari Kolandoto ukiendelea.
Muonekano wa Jengo la vyumba vya madarasa katika Shule ya Sekondari Kolandoto.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, katikati, akiangalia Ramani ya ujenzi wa Shule mpya ya Msingi Ibadakuli, Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Abubakari Gulam, na kulia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi.
Muonekano wa Jengo la Shule mpya ya msingi Ibadakuli manispaa ya Shinyanga.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, mwenye tisheti ya Njano, akiangalia ujenzi chumba cha darasa Katika shule ya Msingi Twendepamoja iliyopo Mwamalili manispaa ya Shinyanga.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, mwenye tisheti ya njano, akiangalia ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Mwangulumbi, iliyopo Kata ya Chibe manispaa ya Shinyanga.
Muonekano wa baadhi ya majengo ya madarasa katika Shule mpya ya Sekondari Mwangulumbi iliyopo Chibe Manispaa ya Shinyanga.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, akishiriki kwenye usafishaji wa eneo la Shule Mpya ya Sekondari Mwangulumbi iliyopo Chibe Manispaa ya Shinyanga.
 

Awali Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, katikati mwenye mavazi ya njano, akiwa kwenye ziara ya kukagua ujenzi wa shule mpya ya Sekondari Mwangulumbi iliyopo Chibe Manispaa ya Shinyanga.

Awali Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, katikati mwenye mavazi ya njano, akisikiliza taarifa ya ujenzi wa vyumba vya Madarasa katika shule ya Msingi Mlimani Old Shinyanga, akisoma taarifa hiyo ni Mwalimu wa Shule hiyo Judith Julius.
Awali Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, katikati mwenye mavazi ya njano, akisikiliza taarifa ya ujenzi wa vyumba vya Madarasa katika shule ya Msingi Mwalugoye, iliyosomwa na Mwalimu wa Shule hiyo Peter Bangili. 
Awali Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, katikati mwenye mavazi ya njano, akiwasisitiza baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Ng'wihando wasome kwa bidii na kutimiza ndoto zao ambapo Serikali inawajengea miundombinu imara ya shule pamoja na kusoma bure.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, mwenye kofia nyeusi, akiwa katika kiwanda cha Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga cha kufyatua Matofali.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, mwenye nguo ya njano, akimpongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi kwa kazi nzuri aliyoifanya ya kusimamia vizuri ujenzi wa vyumba vya madarasa, kushoto ni Mstahiki Meya wa manispaa ya Shinyanga David Nkulila.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, mwenye nguo ya njano, akihitimisha ziara yake kushiriki ujenzi wa vyumba vya madarasa, na kwenda kula chakula kwa Mama lishe kwenye eneo la Soko la Nguzo Nane.
Viongozi wakiendelea kula chakula kwa Mama lishe kwenye eneo la Soko la Nguzo Nane manispaa ya Shinyanga mara baada ya kuhitimisha ziara ya Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, na Ajiram Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, ya kushiriki ujenzi wa vyumba vya Madarasa.

Na Marco Maduhu- Shinyanga.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments