WATOTO WAFARIKI KWA KUANGUKIWA UKUTA MVUA IKINYESHA GEITA

Eneo la ukuta wa nyumba walio kuwemo watoto tisa wa familia moja ambao wawili kati yao walipoteza maisha baada ya kuangukiwa na ukuta wa nyumba yao.

***
Watoto wawili wa familia moja wamefariki dunia baada ya kuangukiwa na ukuta wa nyumba chanzo kikitajwa kuwa ni mvua inayoambatana na upepo iliyonyesha wilayani Geita juzi Jumapili Januari 24, 2021.

Waliofariki ni Asheri Malima(4) na Laurencia Malima (2) waliokuwa wakiishi kijiji cha Kasesa kata ya Kaseme.

Baba wa watoto hao, Malima Kengere amesema aliwaacha wanae tisa nyumbani na kwenda kuuza mahindi ya kuchoma lakini mmoja wa watoto wake alimfuata na kumueleza kuwa nyumba yao imeanguka. Amesema wakati ukuta ukianguka watoto hao walikuwa wenyewe nyumbani.

“Walipoona ukuta unaanguka walikimbia lakini hawa wawili walikuwa wadogo hawakuweza, walifukiwa na kifusi,” amesema akibainisha kuwa siku hiyo mvua ilinyesha kuanzia saa nane mchana hadi saa 10 jioni.

Kamanda wa polisi mkoani Geita, Hendry Mwaibabe amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataka wazazi kuwa waangalifu hasa nyakati za mvua ili kuepuka majanga yanayoweza kuzuilika.

CHANZO- MWANANCHI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments