KOCHA SVEN AIBUKIA KLABU YA F.A.R NCHINI MOROCCO BAADA YA KUTOKA SIMBA SC

Sven Vandenbroeck

KOCHA Sven anatajwa kuibukia ndani ya Klabu ya F.A.R Rabat ya Morocco baada ya kubwaga manyanga ndani ya Klabu ya Simba ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara.

Kocha huyo amesaini dili la miaka miwili kuifundisha timu hiyo baada ya kupata dili nono lililomfanya asepe ndani ya Simba.
Picha ikimuonyesha Sven akisaini mkataba na timu hiyo leo

Vandenbroeck alikuja Bongo msimu wa 2019/20 kupokea mikoba ya Patrick Aussems raia wa Ubelgiji ambaye alifutwa kazi na mabosi wa Simba kwa kile kilichoelezwa kuwa alishindwa kufanya vizuri kwenye Ligi ya Mabingwa baada ya kutolewa na UD Songo hatua ya awali.

Kocha huyo alikiongoza kikosi cha Simba Januari 6 kufuzu hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kubwaga manyanga Januari 7 kwa kile alichoweka wazi kwamba ni masuala ya familia yalimuweka kando na timu hiyo.

Mbeligiji huyo ambaye Mtendaji Mkuu wa Simba, Babra Gonzale anatajwa kuzungumza naye kwa muda wa saa moja ili abaki amekwenda kuchukua nafasi ya kocha Abderrahim Talib ambaye amefukuzwa kazi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post