WATOTO 3,999 WAZALIWA HOSPITALI YA WILAYA YA TARIME, 52 WAFARIKI, 436 WAJIFUNGUA KWA UPASUAJI


Joel Faustin Mkunga Muuguzi Kiongozi wodi ya Wazazi Hospitali ya wilaya ya Tarime
***

Na Dinna Maningo,Tarime
Watoto 3,999 wamezaliwa katika hospitali ya wilaya ya Tarime mkoani Mara kwa kipindi cha Mwezi Januari hadi Desemba 2020 kati ya hao 52 walifariki dunia huku wajawazito 436 wakijifungua kwa upasuaji.

Akizungumza na Malunde 1 blog Mkunga Muuguzi Kiongozi Wodi ya Wazazi katika hospitali ya wilaya ya Tarime Joel Faustin alisema kuwa kila mwezi zaidi ya watoto 300 walizaliwa isipokuwa mwezi Novemba ambapo walizaliwa watoto 285.

Alisema kuwa Wajawazito waliojifungua walikuwa 3,992 ambapo kwa mwezi Januari Wajawazito waliojifungua walikuwa 381,watoto wa kiume waliozaliwa walikuwa 164 na wa kike 217.

Faustin alisema kuwa mwezi Februari Wajawazito waliojifungua 358 watoto wa kiume waliozaliwa 154,wa kike 193,Machi wajawazito 327,wa kiume waliozaliwa 170,wa kike 158, Aprili walikuwa 305,wa kiume waliozaliwa 177,wakike 127,Mei wajawazito 323,wakiume 151,wa kike 169.

"Wajawazito waliofika hospitali kujifungua mwezi Juni walikuwa 341,watoto wa kiume waliozaliwa ni 161,na wa kike ni 176,Julai waliojifungua 316,wa kiume153,wa kike 158, Agosti wajawazito 347,watoto wa kiume waliozaliwa walikuwa 167,wa kike 181",alisema.

Aliongeza kuwa mwezi Septemba waliojifungua walikuwa 314,wa kiume waliozaliwa 151,wa kike 162, Oktoba walikuwa 344,wa kiume waliozaliwa 158,wa kike 150,Novemba wajawazito 285,watoto wa kiume waliozaliwa 151,wa kike 134 na Desemba Wajawazito waliojifungua ni 351,wa kiume  waliozaliwa walikuwa183 na wa kike182.

Faustin alisema kuwa kati ya hao watoto 52 walifariki dunia ambapo mwezi Januari walifariki watoto 3,Februari 7,Machi 5,Aprili 5,Mei 5,Juni 3, Julai 6, Agosti 5, Septemba 3,Octoba 4,Novemba 3 na Desemba 3.

Alisema kuwa wanawake waliofariki dunia wakati wa kujifungua walikuwa sita ambapo mwezi Januari ni 0,Februari 1,Machi-Aprili 0,Mei 1,Juni 2,Julai -Novemba 0 na Desemba 2.

"Katika taarifa ya mwezi tunatakiwa kuhudumia akina mama wanaojifungua 81 lakini tunahudumia zaidi ya 300,tunajitahidi kutoa huduma na kuhakikisha mama anajifungua salama na mtoto anakuwa salama ndiyo maana unaona idadi ya vifo ya watoto na akina mama ni vichache ikilinganishwa na watoto waliozaliwa na akina mama walionifungua",alisema Faustin.

Faustin alisema kuwa kati ya wajawazito waliojifungua,436 walijifungua kwa upasuaji,Januari walikuwa 47,Februari 29,Machi,30,Aprili 40,Mei 34,Juni 37,Julai 42,Agosti 37,Septemba 35,Oktoba 30,Novemba 35 na Desemba 40 na kati ya hao waliokufa ni 3 kati ya vifo 6 vya akina mama waliojifungua.

"Katika kipindi cha mwezi Septemba-Desemba kati ya hao waliozaliwa kulikuwa na watoto njiti 66,mwezi Septemba walizaliwa 15,Octoba 19,Novemba 20 na Desemba 12", alisema Faustin.

Aliongeza kuwa mwezi Desemba 31,walizaliwa watoto 35 kati ya hao wa kiume 15 na wa kike 20,na Januari 1,2021 hadi kufikia saa nane mchana walizaliwa watoto 22 kati ya hao wakiume 12 na wakike 10.

"Kuna watoto wengine walifia tumboni,wengine kutokana na matatizo ya vifaa tiba na dawa kuna watoto wanazaliwa pumzi yao ikiwa ni ndogo unatakiwa kumsaidia pumzi lakini ghafla umeme unakatika inabidi upige simu ili jenereta iwashwe na muda unaenda matokeo yake mtoto anafariki,kuvuja damu nyingi,wajawazito wengine wanakuja wakiwa wamezidiwa kuna mwingine alifia mapokezi alikuja akiwa kazidiwa", alisema Faustin.

Mkunga huyo alitaja baadhi ya sababu za kujifungua kwa upasuaji ni matumizi ya dawa za kienyeji nyumbani,mimba katika umri mdogo,uchungu pingamizi,nyonga kutotoshereza kupitisha mtoto,umri mkubwa wa mimba na watoto kutotanguliza kichwa.

Alisema kuwa uhaba wa dawa na vifaa tiba ni changamoto kubwa kwakuwa mjamzito na watoto wanatakiwa kupata huduma bure lakini hulazimika kununua vifaa tiba na dawa kwa pesa zao jambo ambalo uleta mgongano baina ya wananchi na watoa huduma.

Baadhi ya wananchi akiwemo Paulo Nashoni mkazi wa wilaya ya Rorya aliyekuwa amemsindikiza mkewe kujifungua wameipongeza hospitali hiyo kwa kutoa huduma nzuri ikilinganishwa na miaka ya nyuma" huduma ya sasa ni nzuri ukifika unahudumiwa haraka wahudumu wanatoa lugha zuri tofauti na zamani walikuwa na majibu mabaya,kinachotusumbua ni dawa",alisema.

Simon Olale mkazi wa mtaa wa Kinyambi-kata ya Nkende aliwataka wanaume kuambatana na wake zao wanapokwenda kujifungua badala ya kubaki nyumbani kwakuwa shida inaweza kutokea na akawa msaada huku akiwashukuru watoa huduma kwa kumuhudumia mkewe Esther na kujifungua salama.
Baadhi ya akina mama waliojifungua tarehe 1,Januari 2021 katika hospitali ya wilaya ya Tarime

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post