ALIYEOMBA MTOTO KANISA LA UFUNUO AJIFUNGULIA KANISANI


Mkazi wa mtaa wa Kilimahewa kata ya Bulangwa wilaya ya Bukombe mkoa wa Geita, Justina Lukilisha amejifungua mtoto nje ya kanisa la Ufunuo mjini Ushirombo baada ya kuumwa uchungu ghafla.

Lukilisha amejifungua mtoto wa kike leo Jumapili Januari 3, 2021 akiwa kwenye ibada akidai kuwa hakutegemea uchungu ungemshika kwenye ibada.

Lukilisha amesema anamshukuru Mungu kwa kuwa alifika kwenye ibada kwa ajili ya kumuomba Mungu ili apate mtoto wa kike.

Askofu wa Kanisa la Ufunuo jimbo la Geita, Heryyabwana Majebele amesema mama huyo alikuja na hitaji kubeba mimba tena akiitaji mtoto wa kike na leo kabla ya kuingia kanisani alisema tu anajisikia uchovu lakini ghafla aliumwa uchungu.

Askofu Majebele amesema kwa sasa mama huyo ameenda hospitali ya wilaya ya Bukombe kwa ajili huduma zingine na anaendelea vizuri.

Mkunga kutoka kijiji cha Nyag'holongo wilaya ya Mbogwe, Letisia Komka ambae pia ni muumini wa kanisa hilo amesema mama huyo amejifungua salama.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post