ASILIMIA 85 YA TAMASHA LA KAN KUFANYIKA KWA NJIA YA MTANDAO


Na Woinde Shizza- Arusha
Asilimia 85 ya tamasha la maarifa, sanaa na kujenga mtandao wa kufahamiana (KAN) linatarajiwa kufanyika mtandaoni lengo likiwa ni kuwafikia watu wengi zaidi na kuweza kukabiliana na changamoto ya virusi vya Corona vinayoendelea kuzikabili nchi nyingi duniani.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Tamasha hilo Khalila Mbowe linaloandaliwa na Chuo Cha Maendeleo na ushirikiano wa Kimataifa(MS- TCDC) alisema kuwa kwa miaka miwili ambayo tamasha hilo lilifanyika, kwa asilimia kubwa ilifanyika chuoni hapo lakini kutokana na changamoto inayoikabili dunia hivi sasa asilimia 15 tu ndiyo itakayofanyika katika chuo hicho na asilimia nyingine kufanyika mtandaoni huku washiriki wakitoka katika nchi mbalimbali za bara la Afrika na baadhi kutoka katika mabara mengine.

Bi. Khalila alieleza kuwa pamoja na changamoto hiyo lengo lao la kujimuisha bara zima la Afrika bado lipo pale pale na ndiyo maana yeyote ambaye ni rafiki wa maendeleo na ni rafiki wa Afrika anapaswa kushiriki KAN Festival kupitia mijadala itayoendeshwa katika mitandao ya kijamii na kuona ni hindi gani wanaweza kukuza maendeleo ya bara la Afrika hasa kwa kuangalia ag pplenda ya 2063 ya umoja wa mataifa.

Alisema kuwa tamasha hilo kwa mwaka huu limebeba kauli mbiu isemayo “Maendeleo ya Afrika, mimi nahusika” pia itambatana na mambo mbali mbali ikiwemo mafunzo, mashindano ya ujasiriamali na ubunifu pamoja na mbio zijulikanazo kwa jina la Kan Run ambapo kila mshiriki atashiriki mahali alipo chini ya tamasha hilo.

“Katika hii Kan Run tumeona ni muhimu tunapoongelea maendeleo ya Afrika tushiriki kwa vitendo kwani bila afya nzuri hatuwezi kufanya jambo popote kwa hiyo watakaokuwa eneo hilo mbio hizo zitaanzia hapa lakin kwa walio nje ya hapa watafanya mahali walipo lakin chini ya uwangalizi wetu”, alisema Bi. Khalila.

Aidha alisema kuwa tamasha hilo litaanza Januari 28 hadi 30,2021 ambapo baada ya tamasha hilo watafuatilia kama wote walioshiriki wamehusika mwenye maendeleo ya bara la Afrika kwa namna moja au nyingine.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa chuo hicho Sara Teri alisema kuwa katika kuifikia agenda 2063 wanaangalia wanakujaje kwa pamoja kwenye mambo mbalimbali yakiwemo afya, demokrasia, haki, utawala bora na masuala ya vijana ambapo wameamua wakae kea kwa pamoja na kujadili maendeleo ya Afrika.

“Hili ndio kusudi la KAN Festival na huu ni mwaka wa tatu na inaendelea kukua na kuonekana ulimwenguni na kwa mwaka huu kutakuwa na mijadala tofauti tofauti hapa na kwenya Mitandao pia na lengo ni moja kuhakikisha tunapotoka hapa tunasemaje au tunatokaje Kama washiriki wa mjadala,” alisema Sara Teri.

Alifafanua kuwa mara nyingi watu wa kawaida wanakosa fursa ya kujadili maendeleo ya bara lao na badala yake Kuna kuwa na watu wanaojadili bila sauti za watu wa kawaida kusikika zikionyesa jinsi wanavyoshiriki au kuhusika hivyo lengo ni wewe na yeye mnasemaje juu ya maendeleo ya bara.

Naye mmoja wa wasanii Editha Leonard alisema kuwa kila mtu akisema yeye anahusika utaongeza chachu ya maendeleo kwani kea sasa Afrika ipo sehemu nzuri na ni kivituo cha dunia katika kila nyanja na hii itawafanya Waafrika wazidi kulipenda bara lao.

“Katika tamasha hili mimi binafsi nitaeleze jinsi afya ya akili inavyochangia vifo vya watu kujinyonga Kutokana na kuwa na msongo wa mawazo na kwa kupitia sanaa yangu watu wataona afya ya akili ni jambo la kawaida na kuanza kutafuta ufumbuzi wa kuondoka changamoto hii,” alisema Editha.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments