JIKO LA MKAA LAUA WATU WATANO WA FAMILIA MOJA


Familia nzima ya watu watano imepatikana imeangamia ndani ya nyumba yao mtaani Githurai 45, katika kaunti ya Kiambu nchini Kenya.

Kulingana na polisi, familia hiyo inashukiwa kuvuta hewa yenye sumu ya carbon monoxide kutoka kwa jiko ya mkaa.

 Akithibitisha kisa hicho OCPD Phineas Lingera alisema mwanamume alikuwa muuzaji wa mahindi katika eneo hilo na inashukiwa huenda alikuwa anapika chakula hicho kwenye jiko usiku. 

“Tunaamini alilala sana na kusahau kuzima moto. Familia hiyo huenda ilifariki kutokana na kukosa hewa baada ya kuvuta carbon monoxide,” alisema Lingera. 

Majirani walianza kuwa na wasiwasi baada ya mwanamume huyo kukosa kufungua biashara yaike kama kawaida. Walibisha mlangni pake ambao ulikuwa umefungwa na ndan lakini hawakufunguliwa. Miili imepelekwa katika Hifadhi ya Nairobi City. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments