DC TANO MWERA AHAMASISHA UJENZI WA MADARASA | MALUNDE 1 BLOG

Monday, January 11, 2021

DC TANO MWERA AHAMASISHA UJENZI WA MADARASA

  Malunde       Monday, January 11, 2021
Mkuu wa Wilaya ya Busega Mhe. Tano Mwera ametembelea maeneo mbalimbali wilayani Busega kuhamasisha ujenzi wa vyumba vya Madarasa kwaajili ya kukidhi idadi ya Wanafunzi watakaoingia kidato cha kwanza mwaka 2021. Mhe Mwera amewataka Wananchi kushirikiana na Serikali kuhakikisha Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza wilayani Busega wanaingia kidato cha kwanza na wanapata haki yao ya Elimu.

“Najua tuna upungufu wa madarasa, lakini isiwe sababu ya kuwafanya hawa watoto kukosa haki yao ya Elimu, tutahakikisha sisi serikali kushirikiana na nyie Wananchi tunafanikiwa kujenga madarasa ili Wanafunzi waweze kusoma”, aliongeza Mhe. Mwera.

Kwa upande mwingine Mhe. Mwera amesema Ofisi yake imetoa mifuko 130 kwaajili ya ujenzi na umaliziaji wa madarasa kwenye maeneo yenye mahitaji makubwa ya vyumba vya madarasa wilayani Busega. Aidha Mhe. Mwera ameeleza nia yake ya kuzungumza na wadau wengine wa maendeleo ili kuona uwezekano wa kusaidia ujenzi wa madarasa, huku ameeleza kwamba michango ya Wananchi ni muhimu katika kufanikisha nia ya Wilaya kuweza kukamilisha mahaitaji ujenzi wa madarasa.

Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega Bw. Anderson Kabuko amesema kwamba upungufu wa madarasa umetokana na ongezeko la waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza, ambapo jumla ya Wanafunzi wapatao 5673 wamechaguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka 2021 katika Wilaya ya Busega. Idadi hiyo inafanya upungufu wa madarasa 69 ili kukidhi idadi ya wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza.

“Kwakua kuna madarasa yalishaanza kujengwa katika shule ambazo tayari zina wanafunzi lakini pia kuna baadhi ya shule ni mpya hivyo kama Ofisi tutahakikisha juhudi za kuhamasisha viongozi wa kata na vijiji husika wanamalizia vyumba, hivyo michango iendelee ili kufikia lengo, aliongeza Kabuko”.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post