RAIS MWINYI AIFUNGUA SKULI YA SEKONDARI YA HASNUU MAKAME....ATAKA WANAFUNZI KUSOMA KWA BIDII NA NIDHAMU | MALUNDE 1 BLOG

Monday, January 11, 2021

RAIS MWINYI AIFUNGUA SKULI YA SEKONDARI YA HASNUU MAKAME....ATAKA WANAFUNZI KUSOMA KWA BIDII NA NIDHAMU

  Malunde       Monday, January 11, 2021

 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amewataka wanafunzi kutumia vyema fursa za kuwepo miundombinu bora ya masomo  kwa kusoma kwa bidii na nidhamu.

Dk. Mwinyi amesema hayo  katika Ufunguzi wa Skuli ya Sekondari ya Hasnuu Makame , iliopo Kibuteni Mkoa Kusini Unguja.

Amesema wanafunzi watakaopata nafasi ya kusoma katika skuli hiyo wanapaswa kutumia vyema fursa hiyo kwa kusoma kwa bidii, ili waweze kufaulu katika amsomo yao badala ya  kujihusisha na masuala yatakayosababisha kuharibikiwa katika maisha yao ya baadae.

Alisema ni matumaini yake kuwa wanafunzi watakaosoma skuli hiyo watafulu vyema katika mitihani yao ya Taifa, kw akuwa   skuli hiyo iko katika mazingira mazuri, walimu wazuri pamoja na kuwa na vifaa vya kutosha.

Aidha, aliwataka wakuu wa Wilaya na mikoa kushirikiana na wananchi ili kufanikisha wanafunzi wote watakaotoka katika skuli 34 za Sekondari mkoani humona kujiunga katika Skuli hiyo wanafaulu vizuri.

Vile vile aliwataka walimu kutekeleza ipasavyo wajibu wao wa kusomesha vizuri pamoja na wazazi na walezi kufuatilia maendeleo ya elimu ya watoto wao ili kubaini chanagmoto zinazoweza kujitokeza.Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post