WAZIRI MKUU HANA TAASISI YOYOTE YA MIKOPO....WANANCHI WAJIHADHARI NA MTANDAO BATILI UNAOTUMIA JINA LAKE | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, December 8, 2020

WAZIRI MKUU HANA TAASISI YOYOTE YA MIKOPO....WANANCHI WAJIHADHARI NA MTANDAO BATILI UNAOTUMIA JINA LAKE

  Malunde       Tuesday, December 8, 2020


WANANCHI wametakiwa kujihadhari na ujumbe unaosambazwa kwenye mtandao wa Facebook unaotumia jina la ‘Waziri Mkuu Kassim Majaliwa’ ukiwataka wajasiriamali watume pesa ili wapewe mkopo na taasisi iliyojitambulisha kama Kassim Majaliwa Foundation, kwani mtandao huo ni batili.

Ujumbe huo uonawataka wananchi watume namba za vitambulisho vya kupiga kura ili waweze kupatiwa mkopo anaotaka mkopaji ndani ya saa 24 kwa kutumia namba 0652 940 415. Namba hii imesajiliwa kwa jina la Yunus Milanzi.

Ofisi ya Waziri Mkuu inakanusha kuwepo kwa taasisi hiyo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa hana na wala hahusiki na Taasisi yoyote ya utoaji wa mikopo. Ofisi ya Waziri Mkuu inafuatilia suala hili kwa karibu ili wahusika wote wachukuliwe hatua kali za kisheria.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post