WAADVENTISTA WAHIMIZWA KUCHANGAMKIA FURSA YA MAKAO MAKUU YA NCHI DODOMA KUWEKEZA KATIKA TAASISI ZA ELIMU



Mkurugenzi Idara ya Elimu kanisa la Waadventista Wasabato jimbo kuu la Kusini mwa Tanzania Bi. Devotha Shimbe 

Na Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.

Mkurugenzi Idara ya Elimu kanisa la Waadventista Wasabato jimbo kuu la Kusini mwa Tanzania Bi. Devotha Shimbe amewaasa waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato hapa nchini kuchangamkia fursa ya Kuwekeza elimu kwa kujenga shule katika makao makuu ya nchi Dodoma ili kuwajengea zaidi maadili ya kiroho na yampendezayo Mungu Watoto wa shule za Kiadventista.

Bi. Shimbe amebainisha hayo jijini Dodoma wakati akifanya mahojiano Maalum na Mtandao huu ambapo amesema kanisa linatambua mchango mkubwa unaofanywa na mshiriki mmoja mmoja hivyo ni muhimu washiriki wakawekeza katika suala la elimu hali itakayosaidia kuwaandaa watoto kuwa na maaadili mema kwani elimu ya maadili ya kiadventista ni moja ya uinjilisti.

Hivyo, Bi.Shimbe amebainisha kuwa elimu inayopatikana katika taasisi za elimu za kanisa la Waadventista Wasabato zimejengwa zaidi katika maadili na falsafa ya msingi wa Biblia ambapo watoto huandaliwa katika maisha ya sasa na maisha ya milele.

Aidha, Mkurugenzi huyo wa Idara ya Elimu kanisa la Waadventista Wasabato jimbo kuu la Kusini mwa Tanzania amebainisha kuwa Union ina mpango wa kujenga Chuo kikuu katika makao makuu ya nchi Dodoma ambapo Jumla ya ekari 350 zilishapatikana kwa ajili ya ujenzi huo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments