WAZEE WA MANISPAA YA BUKOBA WASHIRIKI HALFA YA CHAKULA ILIYOANDALIWA NA MBUNGE NEEMA LUGANGIRA

 

MBUNGE wa Viti Maalumu Tanzania Bara kupitia (NGOs) Mhe. Neema Lugangira akizungumza jambo kwa Wazee 38 waliowakilisha Kata zote 14 za  Bukoba Manispaa kwa lengo la hafla fupi ya chakula cha mchana cha pamoja.
Wazee wakimsikiliza kwa umakini MBUNGE wa Viti Maalumu Tanzania Bara kupitia (NGOs) Mhe. Neema Lugangira

MBUNGE wa Viti Maalumu Tanzania Bara kupitia (NGOs) Mhe. Neema Lugangira kushoto akikagua chakula alichopakua Mzee King wa Manispaa ya Bukoba
Baadhi ya Wazee wakipata chakula cha mchana kwenye halfa hiyo iliyoandaliwa na MBUNGE wa Viti Maalumu Tanzania Bara kupitia (NGOs) Mhe. Neema Lugangira
MBUNGE wa Viti Maalumu Tanzania Bara kupitia (NGOs) Mhe. Neema Lugangira kushoto akiwa na Mama Muhazi wakifurahia jambo wakati wa halfa hiyo
MBUNGE wa Viti Maalumu Tanzania Bara kupitia (NGOs) Mhe. Neema Lugangira kulia akiteta jamabo na  REV.Bishop Peter Claver Benjamini ambaye ni mwanzilishi wa NGOs inayoitwa Saidia Jamii ya Wazee Tanzania  (SAWATA) na Saidia Jamii ya Wazee Kagera (SAJAWAKA) na ameshiriki katika uandishi wa Sera ya Taifa ya Wazee
MBUNGE wa Viti Maalumu Tanzania Bara kupitia (NGOs) Mhe. Neema Lugangira (Mb.) katikati wakiwa kwenye picha ya pamoja na wazee hao mara baada ya kupata chakula wakifurahia jambo
***

MBUNGE wa Viti Maalumu Tanzania Bara kupitia (NGOs) Mhe. Neema Lugangira (Mb.) amekutana na Wazee 38 waliowakilisha Kata zote 14 za  Bukoba Manispaa kwa lengo la hafla fupi ya chakula cha mchana cha pamoja. 

Akizungumza wakati akiwakaribisha kwenye hafla hiyo fupi Mhe Neema alisema ameamua kukutana na  wazee hao ambao walifarijika sana huku wakionyesha tabasamu kubwa kutokana na ukarimu ulioonyeshwa na mbunge huyo

Mbunge Neema aliwashukuru wazee hao kwa namna ambavyo walivyomuunga mkono na kumpa ushirikiano mkubwa katika cha Kampeni za Kisayansi na m mchango mkubwa uliopelekea Chama Cha Mapinduzi kupata Ushindi wa Kishindo.

"Kwa kweli niwashukuru sana kwa manufaa ya chama chetu na Taifa kwa ujumla  kwa mchango wenu mkubwa na ninaamini ushirikiano huu utakuwa endelevu na wenye tija kwa manufaa ya chama chetu"Alisema 

Aidha, Mbunge Neema alisema angependa kutumia fursa hiyo pia kuwapa mrejesho kuhusiana na changamoto za wazee walizowasilisha kwake Kipindi cha Kampeni. 

Wakati anawakaribisha kwenye chakula, Mhe Neema Lugangira (Mb.) alitumia fursa hiyo kuwaelezea wazee umuhimu wa Lishe Bora hivyo akawapitisha kwenye menu ya lunch na kila aina ya chakula kina madini na vitamini gani ambazo wanazihitaji zaidi wazee.  

“Wazee wangu mnamahitaji maalumu ya Lishe Bora hivyo tutashirikiana pamoja kuona namna bora ya kuhakikisha mnaongeza ulaji wa mbogamboga na matunda” Alisema

 Wazee wote walimshukuru sana Mhe Neema Lugangira (Mb) kwa kuwakumbuka na kuwafanya wajiskie wana thamani na walimuomba aendelee na utaratibu aliouanzisha wa kukutana na wazee kuwapa mrejesho wa wanayomtuma na walimshauri kuwa utaratibu huo ufanyike kwa ngazi ya Kata ili aweze kufikia wazee wengi zaidi na kupata uelewa wa kina juu ya mahitaji ya wazee. 

 

Katika halfa hiyo Jumla ya Wazee 38 wa Bukoba Manispaa walishiriki ambao walijumuisha wazee wawakilishi kutoka Kata zote 14 za Bukoba Manispaa  na Vijiwe vya Kahawa vya Uswahili na Seneti

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post