VIONGOZI WA DINI 124 MKOANI KAGERA WAPATIWA ELIMU YA LISHE BORA


Mkurugenzi wa Shirika la Agri Thamani Mhe Neema Lugangira (MB) akitoa mafunzo ya lishe bora kwa Viongozi wa Dini kutoka mkoa wa Kagera

 

Mkurugenzi wa Shirika la Agri Thamani Mhe Neema Lugangira (MB) akitoa mafunzo ya lishe bora kwa Viongozi wa Dini kutoka mkoa wa Kagera
Sista Florida Boniface akichangia jambo wakati wa semina hiyo
Sheikh Adinani akichangia jambo kwenye semina hiyo
Padri Hubert Rwebangira akichangia jambo kwenye semina hiyo
Viongozi wa Dini wa mkoa wa Kagera wakifuatilia kwa umakini semina ya Lishe Bora
Viongozi wa Dini wa mkoa wa Kagera wakifuatilia kwa umakini semina ya Lishe Bora

Waratibu wa Kisayansi wakifuatia semina ya Lishe


SHIRIKA la Agri Thamani Foundation limetoa elimu ya Lishe Bora kwa Viongozi wa Dini 124 kutoka Mkoa wa Kagera.

Elimu hiyo inatolewa na Shirika hilo kwa Viongozi wa Dini ikiwa ni moja ya vipaumbele vyake kutokana na viongozi hao kuwa na ushawishi mkubwa kwa jamii.

Akizungumza wakati wa utoaji wa elimu hiyo Mkurugenzi wa Shirika la Agri Thamani Mhe Neema Lugangira (MB) alisema Viongozi wa Dini wana nafasi kubwa ya kuchangia kutokomeza udumavu na utapiamlo kwa ujumla nchini kutokana na nguvu kubwa na ushawishi mkubwa walionao kwa jamii.

Alisema mwaka jana Agri Thamani ilishiriki katika mchakato wa kuingiza Azimio la Lishe katika Maazimio ya Viongozi wa Kitaifa kwenye Kifua Kikuu na Ukimwi. 

Aidha alisema wameanzisha programu ya kutoa Elimu ya Lishe Bora kwa Viongozi wa Dini Ngazi ya Mkoa, Wilaya na Kata ambapo kwa kuanzia mafunzo hayo yamepangwa kufanyika mikoa ya Kagera, Kigoma na Tanga na Viongozi wa Dini kutoka Makundi Yote ya Dini.
 
Kwa umoja wao Viongozi hao wa Dini wameishukuru sana Agri Thamani kwa kupatiwa mafunzo hayo na wamekiri kwamba imewafungua sana na wanakwenda kuhakikisha ajenda ya Lishe Bora inakuwa ajenda yao ya kudumu na ya vitendo.

Hata hivyo wameahidi kufuatilia kwa karibu Utendaji wa Kamati za Lishe za Ngazi husika ambazo wao kama Viongozi wa Dini wanapaswa kuwa Wajumbe.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post