UINGEREZA YAANZA CHANJO YA KUKABILIANA NA JANGA LA VIRUSI VYA CORONA | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, December 8, 2020

UINGEREZA YAANZA CHANJO YA KUKABILIANA NA JANGA LA VIRUSI VYA CORONA

  Malunde       Tuesday, December 8, 2020


 Uingereza leo Jumanne Desemba 8 imeanza kutoa chanjo dhidi ya virusi vya corona, huku bibi kizee wa miaka 90 akiwa wa kwanza kupata chanjo hiyo iliyotengenezwa na Pfizer-BioNTech.


Chanjo hiyo ya kihistoria ilitolewa kwa Margaret Keenan katika hospitali ya Coventry, katikati ya England.


"Najisikia mwenye bahati kuwa mtu wa kwanza kuchanjwa dhidi ya Covid-19," alisema Keenan, ambaye wiki ijayo atafikisha umri wa miaka 91.

Uingereza imeanza zoezi la kutoa chanjo ya Covid-19 iliyotengenezwa kwa ushirikiano wa makampuni ya Pfizer na BioNTech, likiwa taifa la kwanza la Magharibi, kushiriki zoezi hilo kwa umma wa watu wake, katika kile kinachoelezwa uamuzi mkubwa na muhimu wa kukabiliana na janga la virusi vya corona.


Wa kwanza kupata chanjo hiyo katika siku iliyopachikwa jina la "V-Day" walikuwa wazee wenye umri wa kuanzia miaka 80, wafanyakazi wa afya majumbani na wafanyakazi wa afya walio mstari wa mbele.Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post