TATIZO LA MADAWATI LAMALIZWA CHALINZE, RC PWANI, MBUNGE RIDHIWANI WAPONGEZA


Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete (kushoto) akimpongeza mmoja wa walimu waliofika  kupokea madawati kwa shule za Halmashauri ya Chalinze, katikati Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete (kulia) akiwa ameongozana na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo  akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Bi. Zainab Kawawa pamoja na maafisa wengine wakati wa zoezi la kupokea madawati kwa Shule za Halmshauri ya Chalinze
Baadhi ya madawati na viti na meza wakati wa zoezi hilo
Baadhi ya madawati na viti na meza wakati wa zoezi hilo

NA ANDREW CHALE, CHALINZE

HALMASHAURI ya Chalinze, Mkoani Pwani imetekeleza maagizo ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa kutengeza madawati 355, meza na viti 221, huku Mbunge wa Jimbo hilo Ridhiwani Kikwete akichangia shilingi milioni 3.67 kuunga mkono zoezi hilo.

Akizungumza wakati wa kupokea madawati hayo zoezi lilofanyika Mioni Wilayani Bagamoyo, Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete amesema kuwa madawati hayo ni kwaajili ya shule 38, ambapo za Sekondari 20 na shule za msingi 18.

Kikwete  amesema kuwa lengo ni kuhakikisha hakuna mwananfunzi anayekaa chini 

"Lengo letu ni kuona wanafunzi wote wanakaa kwenye madawati ili waweze kuandika vizuri wanapokuwa darasani na kuacha kukaa chini darasani” Amesema Kikwete

Madawati hayo yamepokelewa mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani Evarist Ndikilo na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Bi Zainab Kawawa.

Awali wakati wa kupokea madawati hayo, Mkuu wa Mkoa wa Pwani,  Evarist Ndikilo  aliipongeza Halmashauri ya Chalinze kwa kuvuka lengo la uhaba wa madawati.

"Niwapongeze sana kwa kutimiza lengo la madawati mashuleni. Kwa maana urithi mkubwa kwa watoto wetu ni elimu. Elimu ni msingi bora, elimu ndio kila kitu, elimu ndio urithi.

Mkoa wetu wa Pwani kielimu tunahitaji kuwa nafasi ya kwanza pale juu ama tatu bora kwa maana mwaka 2018 Pwani tulishika nafasi ya  11 kati ya 26,  2019 tulipata nafasi ya 10 na mwaka huu 2020 tumeweza kuwa nafasi ya 9, lengo tufikie pale juu." Alisema Ndikilo 

Aidha, Ndikilopia aliweza kukabidhi madawati hayo na meza na viti kwa wawakilishi wa shule mbalimbali waliofika katika tukio hilo lililofanyika katika viwanja vya shule ya Kikalo, Miono.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments