SERIKALI KUGHARAMIA MAZISHI YA WALIOANGUKIWA NA JUMBA LA MAAJABU ZANZIBAR | MALUNDE 1 BLOG

Sunday, December 27, 2020

SERIKALI KUGHARAMIA MAZISHI YA WALIOANGUKIWA NA JUMBA LA MAAJABU ZANZIBAR

  Malunde       Sunday, December 27, 2020


Serikali imeahidi kugharamia mazishi ya watu wawili waliofariki baada ya kudondokewa na jen-go maarufu la kitalii, Beit Al Ajaib (Jumba la Maajabu) lililopo eneo la Mji Mkongwe mjini Unguja visiwani Zanzibar.

Waliofariki ni Pande Haji Makame (39) na Burhani Ameir Makuno (34) walibainika kati ya saa sita na saa nane usiku kwenye jitihada za kuwatafuta waliofunikwa na kifusi cha jengo hilo.

Wakati wawili hao wakitolewa katika kifusi, wengine wanne walikuwa wakitibiwa majereha waliyoyapata katika Hospitali ya Mnazi Mmoja.

Jumba hilo maarufu lililodumu kwa zaidi ya miaka 130 lilidondoka juzi mchana na kuwafunika mafundi waliokuwa wakilikarabati.

Jana Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla akifuatana na mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya aliwatembelea majeruhi waliolazwa na kwenda eneo la tukio

Katika hatua nyingine, Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi wa haraka ili kubaini chanzo cha kuporomoka kwa sehemu ya jengo la makumbusho la Taifa la Beit al Ajab.

Dk Mwinyi ametoa agizo hilo jana alipotembelea Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja ili kutoa rambirambi kwa wafiwa na kuwapa pole majeruhi wa ajali hiyo.

Amevitaka vyombo hivyo kufanya uchunguzi wa kina haraka ili kubaini chanzo cha kuporomoka kwa jengo hilo na kuleta maafa kwa wananchi ili Serikali ichukue hatua mara moja.Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post