SERIKALI KUBORESHA ELIMU YA UJASIRIAMALI KUINUA SEKTA YA VIWANDA NA BIASHARA HAPA NCHINI

 

Waziri wa Viwanda na biashara Mhe. Geoffrey Mwambe akizungumza wakati kufungua mkutano wa wadau kuhusu rasimu ya sera ya maendeleo ya viwanda vidogo na biashara ndogo hapa nchini uliofanyika Jijini Dodoma. Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Profesa Riziki Mdoe akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau kuhusu rasimu ya sera ya maendeleo ya viwanda vidogo na biashara ndogo hapa nchini uliofanyika Jijini Dodoma. Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Geoffrey Mwambe wa tatu kutoka kushoto waliokaa msitari wa mbele akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa mkutano wa wadau kuhusu rasimu ya sera ya maendeleo ya viwanda vidogo na biashara ndogo hapa nchini mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika Jijini Dodoma.  

Na Ezekiel Mtonyole – Dodoma.

Serikali imesema imejipanga kuboresha elimu ya ujasiliamali kwa wananchi ili kuwajengea uwezo wa kuanzisha biashara ikiwa ni njia mojawapo ya kuwainua wananchi kuwa na wafanyabiashara na wawekezaji wengi hapa nchini.
 
Hayo yamebainishwa Jijini Dodoma na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Geoffrey Mwambe, akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano wa wadau kuhusu rasimu ya sera ya maendeleo ya viwanda vidogo na biashara ndogo ambapo amesema kuwa moja ya vikwanzo vinavyosababisha watanzania kushindwa kupiga hatua kwenye biashara ni ukosefu wa elimu ya ujasiriamali.
 
Ameongeza kuwa pamoja na matatizo ya ukosefu wa masoko ya bidhaa mbalimbali na mitaji lakini elimu bado ni kikwazo kikukwa kwa watanzania katika kuanzisha biashara zao wenyewe.
“Watanzania bado hii elimu ya ujasilimali ni sulaa geni kidogo kwetu leo hii mtanzania anakwenda chuo cha biashara kusoma ili aje kuwa msimamizi wa biashara ya mtu na siyo kubuni yake ”amesema Mhe. Mwambe
 
Amebainisha kuwa kutokana na hali hiyo alivitaka vyuo vya elimu ya biashara nchini pamoja na taasisi mbalimbali kuweka utaratibu wa kutoa mafunzo ya ngazi mbalimbali ili kuwajenga uwezo watu kwenda kuanzisha biashara zao.
 
“Leo hii unakuta chuo cha elimu ya biasahra kama CBE, kinafundisha mtu kwenda kuwa msimamizi wa biashara ya kampuni furani lakini yeye mwenyewe siyo mfanyabiashara inabidi tubadilike hivi karibuni nilikuta na na Mo Dewji akanambia anasoma masters ya biashara Dubai hata sisi wajasiriamali wadogo lazima tusome ili kuwa wafanyabiashara na siyo wasimamizi” amesema.
 
Kuhusu rasimu hiyo ya sera ya maendeleo ya viwanda vidogo na biashara ndogo, amewata wajumbe wa mkutano huo kufanya maboresho ili ipatikane sera itakayo saidia sekta hiyo kukua zaidi hapa nchini.
 
“Lazima mtoke na maboresho ya sera ambayo itakwenda kutambua viwanda vidogo pamoja na biashara ndogo kwani ndizo ambazo zimewatoa watu wengi hapa nchini” amesema.
 
Aidha amefafanua kuwa serikali imekuja na rasimu ya sera hiyo kutokana iliyokuwepo awali kuwa ya muda mrefu na haikidhi mahitaji ya sasa katika ulimwengu wa Sayansi na Taknolojia.
 
“Lakini changamoto nyingine katika sera ile ya awali ni ilijengwa katika malengo ya sekta moja tu ya viwanda ndiyo maana akawa zaidi chini ya SIDO, lakini hivi sasa biashara ndogo zipo katika sekta nyingine pia kama vile mahoteli” amesema.
 
Pia amesema sera hiyo mpya itakuwa na uwezo wa kuwawezesha wajasiriamali wadogo kukuwa kutoka ngazi ya chini na kuwa wafanyabiasahra wakubwa hali itakayo saidia kuongeza walipa kodi na taifa kupata mapato.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments