![]() |
Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya akizungumza jambo katika kikao kazi cha Maofisa Madini Wakazi wa Mikoa yote nchini kilichofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Madini jijini Dodoma. |
![]() |
Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya akizungumza jambo katika kikao kazi cha Maofisa Madini Wakazi wa Mikoa yote nchini kilichofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Madini jijini Dodoma. |
![]() |
Baadhi ya Maofisa Madini Wakazi walioshiriki kikao kazi cha siku tano kilichofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Madini jijini Dodoma |
Na Tito Mselem, Dodoma
Naibu
Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya leo Desemba 18, 2020 amekifunga
rasmi kikao kazi cha siku tano cha Maofisa Madini Wakazi wa Mikoa yote
nchini.
Akifunga kikao
hicho, Prof. Manya amewataka Maofisa Madini Wakazi wa Mikoa yote nchini
kuwa waadilifu katika utendaji wa majukumu yao.
Prof.
Manya, amesema Maofisa Madini wote nchini wanatakiwa kuonesha mfano
kwa kufanya kazi kwa bidii na kwa kufuata taratibu na sheria
zilizowekwa na Serikali ikiwemo kuonesha ubunifu kwenye kazi zao za kila
siku ili kuongeza ufanisi.
Pia,
Prof. Manya, amempongeza Rais Dkt. John Magufuli kwa kumteua kuwa Naibu
Waziri wa Madini kitu ambacho hakuwahi kufikilia katika maisha yake.
“Mheshimiwa
Rais anatamani migodi mipya ifunguliwe nchini na pia Mheshimiwa Rais
anatamani madini yetu ya Makaa ya Mawe yaanze kuchimbwa, hivyo
tuhakikishe tunayafanikisha maono hayo,” alisema Prof. Manya.
Ameongeza
kuwa ndani ya kipindi cha miaka mitatu Prof. Manya amepata nafasi ya
kuteuliwa katika nafasi tano tofauti ambapo January 8, 2017 alichaguliwa
kuwa Kamishina wa Madini, Juni 1, 2018 alichaguliwa kuwa Katibu
Mtendaji wa Tume ya Madini, Desemba 11, 2020 alichaguliwa kuwa Mbunge wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Desemba 11, 2020 alichaguliwa kuwa
Naibu Waziri wa Madini.
Katika
hatua nyingine, Prof. Manya amewapongeza watumishi wote wa Tume ya
Madini kwa ushirikiano mkubwa waliomuonesha katika kipindi chote
alipokuwa akiwaongoza.
Pia,
Prof. Manya ameahidi kumpa ushirikiano na kumshauri Katibu Mtendaji
atakayeteuliwa na Mhe. Rais, kwamba kipaumbele chake kiwe kuelekeza
fedha katika maeneo yanayotoa matokea chanya katika ukusanyaji wa
maduhuli ya serikali.
Aidha,
Prof. Manya amewataka wafanyakazi wote wa Tume ya Madini kusaidiana
katika shughuli zao na kama kuna moja atakosea au atakosa ubunifu katika
shughuli zao inawapasa kusaidiana, kuelekezana na kufundishana ili
kuleta tija katika Sekta ya Madini.
Vile
vile, Prof. Manya amewataka Maofisa Madini Wakazi wa Mikoa yote nchini
kufanya maamuzi ya haki kwa kufuata sheria, taratibu na kanuni
zilizowekwa na Serikali.
“Hakikisheni
mnafanyakazi kwa kuzingatia haki, taratibu na sheria msiwaonee watu
wala msimpendelee mtu, fanyeni kazi kwa juhudi na ueledi ili mlete tija
katika Sekta ya Madini,” alisisitiza Prof. Manya.
Nae,
Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango wa Wizara ya Madini, Augustine
Olel, amewataka Maofisa Madini Wakazi wa Mikoa yote Tanzania kuwa
waadilifu na kufanya kazi kwa kumtanguliza Mwenyezi Mungu na kuwa
waaminifu katika shughuli zao.
Post a Comment