RAIS MAGUFULI AREJESHA FOMU ZAKE ZA MAADILI KATIKA OFISI YA MAKAO MAKUU YA SEKRATARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 31 Desemba, 2020 amewasilisha fomu zake za maadili katika ofisi ya makao makuu ya Sekratarieti ya Maadili ya viongozi Jijini Dodoma.

Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike amekabidhi fomu hizo kwa Kamishna wa Maadili, Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Sivangilwa Sikalalilwa Mwangesi.

Leo ni siku ya mwisho ya kuwasilisha fomu za maadili kwa viongozi wote kwa mujibu wa Sheria namba 13 ya mwaka 1995 ya Maadili ya Viongozi wa Umma


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post