POLISI WANASA WATUHUMIWA 683 MKOANI TABORA WA MAKOSA MBALIMBALI NDANI YA WIKI TATU


NA TIGANYA VINCENT
Jeshi la Polisi limefanikiwa kuwakamata jumla ya watuhumiwa 683 wa makosa mbalimbali Mkoani Tabora katika Oporesheni ilichukua wiki tatu katika Wilaya zote za Mkoa huo.
Kauli hiyo imetolewa  na Mkuu wa Opereshemi Maalumu za Jeshi la Polisi Tanzania Kamishina Mwandamizi wa Jeshi wa Polisi (SACP) Mihayo Msikhela wakati akizungumza na waandishi wa Habari mjini Tabora.

Alisema miongoni mwa watuhumiwa hao ni 277 wamefikishwa Mahakamani na kuhukumiwa , watuhumiwa 255  bado kesi zao zinaendelea na watuhimiwa 42 wako katika uangalizi wa Polisi baada ya kutokuwepo kwa ushahidi madhubuti.

SACP Msikhela alisema baadhi ya vielelezo vilivyokamatwa ni silaha aina ya gobore moja, mapanga tisa, meno ya tembo mawili, pikipiki 34 , magodoro 10 na simu za mkononi nne.

Vitu vingine vilivyokutwa kwa watuhimiwa ni vyuma vya reli viwili,runinga za aina mbalimbali 19, mfano wa sare za majeshi mbalimbali ya ndani na nje na pombe haramu ya gongo lita 408.

Aliongeza kuwa miongoni mwa watuhumiwa hao wamefanikiwa kukamata raia wa nje kabila Mhutu akiwa na aina mbalimbali za mfano wa sare za Polisi na majeshi mengine.

SACP Msikhela alisema mtuhumiwa huyo akikamatwa baada ya Askari Polisi kumuona amevaa sare ambazo zinafanana na za Polisi lakini mshono wake ni tofauti.

Alisema baada ya kupekua begi alililokuwa amebeba ndipo walikuta sare zinazotaka kufanana na zile za Jeshi la Wananchi na nyingine zinafana na za Majeshi ya Nje.

SACP Msikhela alisema katika operesheni hiyo ya kuanzia tarehe 7 mwezi huu wamebaini kuwa magenge yanayojihusisha ni uvunjaji , uporaji, na wizi ni vijana ambao umri wao ni kuanzia miaka 15 hadi 21.

Alisisitiza Jeshi la Polisi litaendelea kufanya opresheni na misako ya mara kwa mara kwa kushirikiana na raia wema ili kukomesha uhalifu mkoani Tabora.

MWISHO


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments