MWANDISHI ALIYERIPOTI MLIPUKO WA CORONA CHINA AHUKUMIWA JELA MIAKA MINNE | MALUNDE 1 BLOG

Monday, December 28, 2020

MWANDISHI ALIYERIPOTI MLIPUKO WA CORONA CHINA AHUKUMIWA JELA MIAKA MINNE

  Malunde       Monday, December 28, 2020


Mwandishi wa habari Zhang Zhan amehukumiwa kifungo cha miaka minne kwa kuripoti mlipuko wa kwanza wa virusi vya Corona katika mji wa Wuhan. Hukumu hiyo imetolewa na mahakama ya Shanghai.

Mahakama ya Shanghai imechukua uamuzi kifungo cha miaka minee dhidi ya mwandishi wa habari Zhang Zhan baada ya kuangazia mlipuko wa kwanza wa virusi vya Corona, amesema mwanasheria wake.

Kwa mujibu wa mashataka yanayomkabili, alisafiri hadi Wuhan mwezi Februari kuripoti kuhusu mlipuko wa virusi bila kuzingatia kanuni zilizowekwa.

Ripoti yake aliyoweka mubashara katika mtandao wa kijamii ilivuma sana mwezi Februari, ilimweka mashakani baada ya kuvutia mamlaka za China.

Kesi yake, ambayo imefunguliwa Jumatatu hii, ilichukua saa chache kbala ya kutolewa uamuzi. Mwandishi huyo wa habari, mwenye umri wa miaka 37, alikamatwa mwezi Mei mwaka huu, akishumiwa "kuchochea vurugu" kwa kueneza "habari za uwongo".Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post