NDUGAI AMWAPISHA MBUNGE MTEULE ALIYETEULIWA KUWA NAIBU WAZIRI WA MADINI

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai, amemuapisha Profesa Shukrani Manya kuwa Mbunge wa Bunge hilo.

Profesa Manya ameteuliwa mapema hii leo na Rais John Magufuli kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na pia ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Madini.

Kabla ya uteuzi huo, Profesa Manya alikuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini Tanzania


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post