KAMPENI YA CHANJA KIJANJA NA EXIM MASTERCARD YAJA KIVINGINE

Mkuu wa huduma ya rejareja wa benki ya Exim, Andrew Lyimo ( Katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kutangaza maboresho zaidi ya kampeni ya benki hiyo ijulikanayo kwa jina la ya 'Chanja Kijanja na Exim Mastercard' inayolenga kuhamasisha wateja wa benki hiyo kutumia kadi katika manunuzi ya mtandaoni au kufanya malipo kupitia mashine za malipo (POS). Wengine ni pamoja na Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo Bw Stanley Kafu (Kushoto) na Mkuu wa Idara ya Kidigitali na huduma Mbadala wa benki hiyo Bw Silas Matoi.


Kampeni ya 'Chanja Kijanja na Exim Mastercard' inayolenga kuhamasisha wateja wa benki hiyo kutumia kadi katika manunuzi ya mtandaoni au kufanya malipo kupitia mashine za malipo (POS) imechukua sura mpya huku zawadi kwa washindi mbalimbali wa kampeni hiyo zikiongezwa.

Kampeni hiyo inatoa fursa ya kipekee kwa wateja wa benki hiyo kufurahia huduma zinazokwenda sambamba na mfumo wa maisha yao kupitia benki hiyo.

Kwa mujibu wa mkuu wa kitengo cha wateja wadogo na kati wa Benki ya Exim Tanzania, Bw. Andrew Lyimo, alisema kupitia kampeni hiyo washindi sasa watajipatia zawadi mbalimbali ikiwemo pesa taslimu za ada ya shule kwa mtoto pamoja na vifaa vyote vya shule.

“Kwa kuheshimu vipaumbele na matakwa ya washindi wetu, kupitia kampeni hii sasa tunatoa uhuru kwa washindi watatu wajichagulie wenyewe zawadi zao ikiwemo kwenda Serengeti au kwenda visiwani Zanzibar wakiwa na wenza wao huku kila kitu kikiwa kimelipiwa au hata zawadi ya pesa taslimu ya ada ya shule kwa mtoto mmoja pamoja na vifaa vyote vya shule.’’ Alisema.

Alibainisha kuwa wakati wa kampeni hiyo, jumla ya washindi 10 wa kila wiki watapata zawadi za vocha za manunuzi zenye thamani ya shilingi 50,000 huku kila mwezi washindi watano (5) watazawadiwa simu janja (smartphones).

"Kama ilivyokuwa awali, kutakuwa na zawadi za kila wiki, kila mwezi na kubwa za mwisho wa kampeni. Wanachotakiwa wateja wetu ni kufanya miamala yao kupitia kadi ya Exim Bank MasterCard mara nyingi iwezekanavyo kwa kuwa kila muamala unaongeza nafasi moja ya kushinda,'' aliongeza.

Kwa mujibu wa Bw. Lyimo, Kampeni hiyo ipo wazi kwa wateja wote wanaomiliki kadi za Exim Bank MasterCard, pamoja na wateja wote ambao wameomba au wataomba kadi mpya katika kipindi cha kampeni.

"Kwa upande wetu Benki ya Exim, wateja wanaotumia kadi zetu wamekuwa wakifurahia urahisi wanapofanya manunuzi au malipo kwenye ya mahitaji muhimu kwenye maduka (Shopping), ununuzi wa bidhaa kimataifa kupitia mtandaoni mfano Amazon, Ebay, Alibaba, Jumia, Kikuu, Duka direct, malipo wakati wa safari, malipo ya hoteli na shughuli za kitalii. '' Alisema.

Naye Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo Bwana Stanley Kafu, alielezea kufurahishwa kwake na mwitikio mkubwa wa kampeni hiyo akisema, "Tumefurahishwa sana na mapokeo ya kampeni ya Chanja Kijanja. Maboresho tuliyoyafanya kwenye kampeni hii yanasadifu ubora wa huduma za kibenki kwa wateja wetu, na hiyo ndio falsafa ya kiutendaji hapa benki ya Exim'' alisema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments