CHADEMA YAZUNGUMZIA RUFAA YA HALIMA MDEE NA WENZAKE


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) nchini Tanzania kimesema, Halima Mdee na wenzake 18 bado hawajawasilisha rufaa zao za kupinga kufukuzwa uanachama wa chama hicho.
 

Chadema imetoa taarifa hiyo jana Alhamisi tarehe 3 Desemba 2020 ikiwa zimepita siku mbili tangu Mdee na wenzake hao kutangaza kukata rufaa Baraza Kuu kuoinmga uamizi wa kamati kuu wa kuwafukuza.

Mdee na wenzake 18, walifukuzwa Chadema kwa tuhuma za usaliti, kughushi na kujipeleka bungeni kuapishwa tarehe 24 Novemba 2020 na Spika Job Ndugai kuwa wabunge wa viti maalum, wakijua chama hicho, hakijapendekeza majina yao Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Uamuzi wa kamati kuu, ulitolewa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe tarehe 27 Novemba 2020 akisema, Mdee na wenzake wamekisaliti chama na kama hawaridhiki na uamuzi huo wa kuwafukuza, wanaweza kukata rufaa baraza kuu ndani ya siku 30 au kuomba radhi.

Tarehe 1 Desemba 2020, Mdee na wenzake 18 wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, walisema hawana lengo la kuondoka ndani ya chama hicho na watabaki kama ‘wanachama wa hiari’ wakati mchakato wa kukara rufaa ukiendelea.

 



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments