BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI: SURA MPYA ZATAWALA, WENGI NI VIJANA | MALUNDE 1 BLOG

Sunday, December 6, 2020

BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI: SURA MPYA ZATAWALA, WENGI NI VIJANA

  Malunde       Sunday, December 6, 2020

 Rais wa Tanzania,  John Magufuli  jana Jumamosi Desemba 5, 2020 amefanya uteuzi wa mawaziri 21 na naibu mawaziri 23 huku akiwateua waliokuwa makatibu wakuu wa wizara kuwa wabunge na kisha kuwateua kuwa mawaziri.


Pia  ameanzisha wizara mpya ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na kumteua mbunge wa Kigamboni, Dk Faustine Ndugulile kuwa waziri wa wizara hiyo na Kundo Mathew kuwa naibu waziri.

Akitangaza uteuzi huo katibu mkuu kiongozi, Balozi John Kijazi amesema uteuzi wa mawaziri wawili, Profesa Palamagamba Kabudi (Mambo ya Nje) na Dk Philip Mpango (Fedha) unaendelea na hivyo kufanya idadi ya mawaziri kuwa 23 na naibu mawaziri 23.

Walioteuliwa kuwa wabunge na kisha uwaziri ni Dk Dorothy  Gwajima aliyekuwa naibu katibu mkuu Tamisemi akishughulikia sekta ya afya pamoja na Dk Leonard Chamuriho ambaye alikuwa katibu mkuu Wizara ya Uchukuzi.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post