MUUAJI HATARI WA KUVIZIA MAKAHABA AFARIKI DUNIA


Samuel Little, mtu aliyetajwa na shirika la kijasusi la FBI kama muuaji mkubwa wa kuvizia katika historia ya Marekani amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 80.

Little alifariki dunia katika hospitali ya mjini California siku ya Jumatano, idara ya magereza imesema. Alikuwa akihudumia kifungo cha mauaji ya wanawake watatu.

Lakini kabla ya kifo chake , alikuwa amekiri kuwaua wanawake 93 kati ya mwaka 1970 na 2005.

'Little aliwalenga watu waliokuwa hawawezi kujitetea, wengi wao wakiwa makahaba ama watumiaji wa mihadarati' , walisema maafisa.

Akiwa Bondia wa zamani , Little angewaangusha waathiriwa wake kwa kuwapiga ngumi kabla ya kuwanyonga - ikimaanisha kwamba hakukuwepo ishara zozote , kama vile kuwadunga kisu ama kuwapiga risasi na kwamba mtu huyo alikuwa ameuawa.

Badala yake vifo vyake vingi vilidaiwa kula dawa kupitia kiasi ama vya ajali na havikuchunguzwa.

Baadhi ya miili haijapatikana , kitengo hicho kilisema.

Mwaka uliopita FBI lilisema kwamba wachambuzi wake walisema kwamba madai yote aliokiri kutekeleza yalikuwa ya kweli.

Pia walitoa picha za waathiriwa aliowachora wakati akiwa jela katika jaribio la kuwatafuta aliowaua.
Shirika la FBI lilitoa michoro ya Samuel Little kwa matumaini kwamba waathiriwa watatambulika.

Little alikamatwa mwaka 2012 kwa mashtaka ya kutumia mihadarati mjini Kentucky na kusafirishwa hadi California, ambapo maafisa walitafuta vinasaba vyake .

Tayari alikuwa na rekodi mbaya ya uhalifu akiwa na mashtaka ya wizi wa mabavu hadi ubakaji katika maeneo mbalimbali Marekani.

Vinasaba vya DNA vilimuhusisha na mauaji ya watu watatu ambao hayajatatuliwa kutoka 1987 na 1989 katika kaunti ya mji wa Los Angels.

Alikataa kufanya makosa lakini hatimaye alipatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo cha maisha , bila fursa ya kuachiliwa katika siku za usoni.

CHANZO - BBC SWAHILI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post