JPM AMUAGIZA JAFO AANZE NA MKURUGENZI WA GEITA ALIYENUNUA GARI LA MIL 400 | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, December 9, 2020

JPM AMUAGIZA JAFO AANZE NA MKURUGENZI WA GEITA ALIYENUNUA GARI LA MIL 400

  Malunde       Wednesday, December 9, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli amemuagiza Waziri wa Ofisi ya Rais -Tamisemi, Suleiman Jaffo kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Geita Mhandisi Modest Aporinary kutokana na matumizi mabaya ya fedha za Serikali Sh Milioni 400 zilizolenga kuhudumia wananchi lakini akanunua gari la kutembelea.

 Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo Jumatano wakati akiwaapisha Mawaziri na Naibu Mawaziri Ikulu Chamwino Dodoma.

“TAMISEMI kuna matumizi mabaya ya fedha Jafo Suleiman  Waziri wa TAMISEMI umefanya vizuri sana lakini kwenye kudhibiti fedha bado, nimefikiria sana kukurudisha au kutokukurudisha",amesema Rais Magufuli.

 "Hapo nataka kusema ukweli tuelewane hili la matumizi mabaya. Unakuta mkurugenzi ananunua gari la milioni 400 fedha tumehangaika nazo kuzipata wananchi, watoto wanachangishwa unakuta madawa hayatoshi. Nataka kazi yako ya kwanza kwenda kumsimamisha mkurugenzi wa Geita ndiyo kazi yako ya kwanza ukaanze nayo", amesema
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post