WANAFUNZI WA VYUO VIKUU WAHIMIZWA KUJIUNGA NA AKADEMI YA TEHAMA YA HUAWEI


Mwakilishi kutoka kampuni ya HUAWEI, Bw George Harrison akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha DIT,alipotembelea chuoni hapo, jijini Dar es Salaam jana kuelezea program ya Huawei ya kuendesha bure masomo ya ICT ( Huawei ICT Academy) inayoendeshwa katika vyuo mbalimbali hapa nchini. 
Mwalimu wa Chuo cha DIT Jumanne Ally akiwaelezea kuhusu vifaa vya maabara mpya ya TEHAMA wanafunzi wa chuo hicho, waliyowekewa na kampuni ya HUAWEI chuoni hapo kwaajili ya kujifunza mambo mbalimbali kuhusina na kile wanachosomea,vwapili kutoka kulia ni mwakilishi wa kampuni ya HUAWEI, George Harrison.
***

Wito umetolewa kwa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini kuchukua nafasi za kujiandikisha bure kwenye Akademi za TEHAMA za Huawei zinazoendeshwa katika vyuo vikuu kadhaa nchini.

Akizungumza wakati wa kukaribisha wanafunzi wapya wa masomo ya TEHAMA na wanafunzi wanaoendelea kufanya masomo katika ngazi tofauti, Jumanne Ally, ambaye ni Mhadhiri msaidizi katika Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT) katika Idara ya Mawasiliano alisema wanafunzi kadhaa ambao walipitia akademi za Huawei tayari wameshaajiriwa katika kampuni mbali mbali za mawasiliano na simu hapa nchini.

Wengine, kama alivyosema kwa upande wake, wamefanikiwa kujiajiri na kuunda njia za masoko kwa ajli ya kujiingizia kipato.

“Baada ya wanafunzi kufaulu mitihani yao ya TEHAMA ambayo hufanyika mtandaoni, wanapewa vyeti vya taaluma ambavyo huwasaidia kutambulika kama waatalamu kwenye fani hiyo kote duniani.” Alisema

Wanafunzi pia walipata nafasi ya kutembelea maabara ya TEHAMA ya Huawei katika Chuo cha DIT iliyopo katika majengo ya chuo hicho. Maabara hiyo ina vifaa vipya vya kisasa vya Huawei na ilifunguliwa rasmi mwaka jana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

George Harrison, Afisa wa Huawei, alisema kuwa kampuni yake pia inatoa vifurushi vya bure vya mtandao kwa wanafunzi ambao wamejiandikisha katika programu hiyo kupata habari zinazohusiana na ICT, kupata maelezo na kufanya mitihani yao mtandaoni.

“Wanafunzi wa TEHAMA ambao wameandikishwa katika akademi za Huawei pia wanapata nafasi ya kushiriki mashindano ya TEHAMA yaliyofadhiliwa kikamilifu yaliyofanyika katika ngazi za kikanda, Afrika na kimataifa ambapo Tanzania ilikuwa imeibuka washindi wa pili katika kiwango cha ulimwengu kushinda nchi zingine zilizoendelea sana kiteknolojia.” George Harrison.

Huawei pia huandaa kile kinachoitwa Maonyesho ya Kazi ya TEHAMA ambayo wanafunzi wa TEHAMA kutoka vyuo tofauti wanapata nafasi ya kuchangamana na kampuni za mawasiliano ili kupata fursa za ajira na wengine kwa mahusiano ya kikazi.

Rodrick Simon, ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa pili katika chuo cha DIT, akichukua digrii ya Elektroniki na Mawasiliano ya simu alisema kuwa yeye ni mmoja wa wanafunzi ambao wameandikishwa katika akademi ya TEHAMA ya Huawei.

"Ni akademi bora sana ambayo inaendeshwa na Huawei," Tumeingizwa katika ulimwengu wa TEHAMA na vifaa vya kisasa vya Huawei, tukitegemea teknolojia mpya. Kwa mara ya kwanza, nilijiandikisha katika Cheti cha Huawei cha Kiwango cha Kwanza cha mshirika wa TEHAMA, lakini sikufaulu mtihani huo. Niliirudia mara nyingine tena na kufanikiwa kufaulu na kupata cheti cha utaalam cha Huawei, mipango yao ni rahisi sana," alisema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments