WATU WATATU WAFA MAJI ZIWA VICTORIA

Kamanda wa polisi mkoa wa Simiyu Richard Abwao

Na Samirah Yusuph - Busega
Watu watatu wakazi wa wilaya ya Busega Mkoani Simiyu ambao ni wavuvi katika ziwa Victoria wamekufa maji kwa kuzama maji baada ya mtumbwi waliokuwa wanautumia katika shughuli zao kupasuka.

Tukio hilo limetokea jana tarehe 29 mwezi wa 11 katika kata ya Kabita tarafa ya Busega wakati wavuvi hao wakiwa wanaendelea na shughuli zao za uvuvi kama kawaida.

Kamanda wa polisi mkoa wa Simiyu Richard Abwao amesema kuwa kwa mujibu wa taarifa ya daktari aliyechunguza miili hiyo kifo chao kilitokana na kunywa maji mengi na kukosa hewa.

"Waliokufa maji ni Mnaga Manyama miaka 28, Kulwa Juma miaka 15 na Bitulo Manyama wote wakazi wa Kabita wilayani Busega.

Aidha tukio hilo lilitokea baada ya mtumbwi waliokuwa wanatumia kuzama kufuatia mtumbwi huo kupasuka na kuanza kuingiza maji",alisema Abwao.

Ametoa wito kwa wananchi wanaofanya shughuli za uvuvi kufanya ukaguzi na matengenezo hitajika ya vifaa vyao mara kwa mara.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post