KATAMBI AANIKA MIKAKATI KULETA MAPINDUZI SHINYANGA...."SITACHEKA NA ANAYEKWAMISHA MAENDELEO"

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi 

Na Kadama  Malunde - Malunde 1 blog

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi amesema amejipanga kikamilifu kuhakikisha anatekeleza ahadi zote alizozitoa wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu 2020 huku akisema hatowavumilia wale wote wenye nia ya kutaka kumkwamisha katika malengo yake ya kuwaletea maendeleo wananchi.

Katambi ameyasema hayo leo Jumatatu Novemba 30,2020 wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga kwenye kikao kilichohudhuria pia na Mstahiki Meya Mteule wa Manispaa ya Shinyanga, Mhe. David Nkulila,Madiwani na viongozi wa CCM.

Katambi amesema kipindi cha uchaguzi kimeisha hivyo kinachotakiwa sasa ni kuchapa kazi ili kuondoa kero zinazowakabili wananchi kuwaondolea maumivu waliyonayo.

“Mimi Mbunge kwa kushirikiana na madiwani,viongozi wa chama na serikali pamoja na wananchi hatutakuwa tayari kucheka na mtu ambaye hatatekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM. Kwa kweli hatutakuwa na simile na atakayetukwamisha”,amesema Katambi.

“Shinyanga tunahitaji maendeleo,tunataka kuubadilisha mkoa huu lakini pia kuifanya Manispaa ya Shinyanga kuwa Jiji. Haiwezekani mkoa huu mama unazidiwe maendeleo na mkoa wa Simiyu,lazima sasa tuupe heshima mkoa huu. Pia kula fedha ya serikali ni marufuku”,ameeleza Katambi.

Katambi amesema sasa ni wakati wa kutekeleza ahadi alizoahidi ikiwa ni pamoja na kuboresha sekta ya kilimo,kujenga soko la kisasa, stendi ya kisasa,kiwanda cha nyama na ajira.

 Katika hatua nyingine amesema kuanzia wiki ya pili ya Mwezi Desemba ataanza kufanya ziara kwenye kata kwa ajili ya kuwaeleza wananchi kuhusu mipango mikakati aliyoweka katika kutekeleza ilani ya CCM.

Kwa upande wake, Mstahiki Meya Mteule wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Mhe. David Nkulila amesema amejipanga kusimamia nidhamu ya fedha katika halmashauri hiyo na kwamba hatakubali kuona malalamiko juu ya miradi yanaendelea kuwepo.

“Maendeleo yote yanahitaji fedha,ni lazima tuwe na nidhamu ya fedha. Nitafanya kazi usiku na mchana nikishirikiana na madiwani, mbunge, viongozi wa chama na serikali pamoja wananchi ili kuhakikisha tunaleta maendeleo katika jamii”,amesema Nkulila.

“Mkuu yeyote wa Idara katika halmashauri atakayethubutu kutukwamisha itabidi atupishe. Sitakubali malalamiko yaliyokuwepo yaendelee kuwepo na hatutasubiri hadi kiongozi wa kitaifa kuja kututatulia kero zetu”,ameongeza Nkulila.

Naye Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Abubakari Gulam Mukadam amesema Chama Cha Mapinduzi kimejiandaa kutekeleza Ilani ya CCM kwa kasi kubwa kwa asilimia 100 na kwamba madiwani na mbunge watapanga siku maalumu kwa ajili ya kusikiliza kero na matatizo ya wananchi.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Novemba 30,2020 wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Novemba 30,2020 wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga.
Mstahiki Meya Mteule wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Mhe. David Nkulila akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Novemba 30,2020 wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga.
Mstahiki Meya Mteule wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Mhe. David Nkulila akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Novemba 30,2020 wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Abubakari Gulam Mukadam akizungumza na waandishi wa habari leo
Diwani wa kata ya Mwawaza Juma Nkwabi akielezea namna alivyojipanga kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM.
Katibu wa Siasa na Uenezi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Said Bwanga  akielezea namna CCM ilivyojipanga kuwaletea maendeleo wananchi.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post