TAKUKURU na Mkurugenzi wa jiji Dar waokoa bil. 12 ujenzi wa stand ya Mbezi Luis
Saturday, November 14, 2020
Mkurugenzi mkuu Takukuru, Brigedia John Mbungo amesema ofisi yake kwa kushirikiana na mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Zipora Liana wamedhibiti Sh12 bilioni ambazo zingelipwa kinyume na mipango katika mradi wa ujenzi wa stendi mpya ya mabasi mkoa wa Dar es Salaam.
Mbungo ameeleza hayo leo Jumamosi Novemba 14, 2020 katika mkutano wake na waandishi wa habari.
Amesema fedha hizo zilikuwa zinalipwa kwa makandarasi kama ziada kwa kazi ambayo haikufanyika.
"Udhibiti huu umefanikiwa kwa kuwa na wachunguzi na wataalamu wa ujenzi kutoka Takukuru waliokuwa wakifuatilia kazi hii kwa karibu,” amesema.
Mbungo ametoa pongezi kwa Liana huku akitoa wito kwa wakurugenzi wengine kuendelea kushirikisha na taasisi hiyo kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kuhakikisha fedha za Serikali zinazotokana na kodi za wananchi zinatumika kulingana na malengo yaliyowekwa.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com
🚧🚦 Usiendeshe gari lako bila Mafunzo na Leseni halali_ 📲 Wasiliana nasi sasa: wa.me/255740273285 Unahitaji nini? 🚘 Unataka kujifunza udereva wa magari na kupata Cheti? 📄 Una cheti unataka kupata Leseni? 🔄 Unajua kuendesha lakini huna cheti wala leseni na unataka refresh upate cheti? 🛣️ Una nyaraka zote muhimu lakini unahitaji kujifua zaidi barabarani? ✅ Una Leseni bila cheti na unataka renew? 🌍 Tupo mikoa yote Tanzania hadi vijijini! 📞 Tupigie sasa: 0769 763 285
Social Plugin