Picha : RC CHALAMILA AFUNGA TAMASHA LA 6 LA JINSIA MBEYA..ASEMA "TUTASHUGHULIKA NA WANAOFANYA UKATILI KWA WANAWAKE NA WATOTO"


Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mhe. Albert Chalamila.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mhe. Albert Chalamila amefunga Tamasha la sita la Jinsia Ngazi ya Wilaya lililoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) lililokuwa linafanyika katika uwanja wa Kijiji cha Hatwelo kata ya Ijombe Halmashauri ya wilaya ya Mbeya Novemba 18,2020 hadi leo Novemba 20,2020.

Tamasha hilo lenye Kauli Mbiu ya “Miaka 25 ya Beijing : Tusherehekee, Tutafakari, Tujipange, Tusonge Mbele, Twende pamoja” limekutanisha wadau wa haki za wanawake na watoto zaidi ya 400 kutoka mikoa 9 nchini ambayo ni Shinyanga, Mara, Tanga, Dar es salaam, Mbeya,Kilimanjaro,Dodoma, Mtwara na Kigoma. 

Akizungumza wakati wa kufunga Tamasha hilo leo, Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mhe. Albert Chalamila amewataka wanawake kujiona ni wa thamani na kusimama imara na kuachana na mtazamo kuwa mwanaume ndiyo anatakiwa afanye kila kitu katika familia. 

Chalamila amesema serikali inaendelea kuboresha hali ya maisha ya wanawake ili kufikia usawa wa kijinsia ikiwa ni pamoja na kuwawezesha kiuchumi kwa kuwapatia mikopo kupitia halmashauri za wilaya. 

“Wanawake simameni imara bila kufifisha thamani yenu, mwanamke siyo mtu wa ndiyo ndiyo tu kwa kila kitu. Msijirahishe rahishe na kukubali rushwa ya ngono.Tafuteni fursa za uongozi huku mkitambua kuwa mwanamke akiwa katika nafasi salama basi kizazi chote kimepona”,amesema Chalamila. 

Mkuu huyo wa mkoa pia amekemea vitendo vya wanaume kudhulumu mali wanawake na kwamba serikali haipo tayari kuona wanawake na watoto wakionewa na kunyanyaswa huku akisisitiza kuwa serikali itawashughulikia wote wanaojihusisha na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Pia ametaka wanawake kutoa taarifa pale wanapotendewa vitendo vya kikatili ili hatua za haraka zichukuliwe dhidi ya wahusika. 

Katika hatua nyingine Chalamila amesema mkoa wa Mbeya bado unakumbwa na matukio ya unyanyasaji dhidi ya watoto ikiwemo ubakaji na kukata sehemu za siri za watoto matukio ambayo yanahusishwa na imani za kishirikiana hivyo kuitaka jamii kuachana na vitendo hivyo 

Chalamila ametumia fursa ya Tamasha hilo kuupongeza Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa namna unavyoshirikiana na serikali katika kupigania haki za wanawake na watoto. 

"TGNP mmekuwa wadau wakubwa katika mkoa wa Mbeya,mmeisaidia sana serikali kufanya mambo ambayo yalipaswa kufanywa na serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi",amesema.

Mjumbe wa Bodi ya TGNP, Jovitha Mlay amesema tamasha 6 la Jinsia limeshirikisha wadau wa haki za wanawake na watoto wanaofanya kazi na TGNP kutoka mikoa tisa nchini
ambapo washiriki wamejadili kwa kina kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo Uandaaji wa bajeti yenye mrengo wa kijinsia kwa ujenzi wa TAPO, Wanawake na Uongozi,Ukatili wa kijinsia,Haki ya mazingira na mabadiliko ya tabianchi na mtoto wa kike, teknolojia na ubunifu. 
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mhe. Albert Chalamila akizungumza wakati wa kufunga Tamasha la sita la Jinsia Ngazi ya Wilaya lililoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) katika uwanja wa Kijiji cha Hatwelo kata ya Ijombe Halmashauri ya wilaya ya Mbeya  leo Ijumaa Novemba 20,2020. Wa kwanza kulia ni Chifu wa Kabila la Wasafwa mkoa wa Mbeya, Roketi Mwanshinga akifuatiwa na Mjumbe wa Bodi ya TGNP, Jovita Mlay. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mhe. Albert Chalamila akizungumza wakati wa akifunga Tamasha la sita la Jinsia Ngazi ya Wilaya lililoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) katika uwanja wa Kijiji cha Hatwelo kata ya Ijombe Halmashauri ya wilaya ya Mbeya leo Ijumaa Novemba 20,2020.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mhe. Albert Chalamila akizungumza wakati wa akifunga Tamasha la sita la Jinsia Ngazi ya Wilaya lililoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) katika uwanja wa Kijiji cha Hatwelo kata ya Ijombe Halmashauri ya wilaya ya Mbeya  leo Ijumaa Novemba 20,2020. 
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mhe. Albert Chalamila akizungumza wakati wa akifunga Tamasha la sita la Jinsia Ngazi ya Wilaya lililoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) katika uwanja wa Kijiji cha Hatwelo kata ya Ijombe Halmashauri ya wilaya ya Mbeya  leo Ijumaa Novemba 20,2020. 
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mhe. Albert Chalamila akizungumza wakati akifunga Tamasha la sita la Jinsia Ngazi ya Wilaya lililoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) katika uwanja wa Kijiji cha Hatwelo kata ya Ijombe Halmashauri ya wilaya ya Mbeya  leo Ijumaa Novemba 20,2020. 
Mjumbe wa Bodi ya TGNP, Jovita Mlay akizungumza wakati wa kufunga Tamasha la sita la Jinsia Ngazi ya Wilaya lililoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) katika uwanja wa Kijiji cha Hatwelo kata ya Ijombe Halmashauri ya wilaya ya Mbeya  leo Ijumaa Novemba 20,2020. 
Mjumbe wa Bodi ya TGNP, Jovita Mlay akizungumza wakati wa kufunga Tamasha la sita la Jinsia Ngazi ya Wilaya lililoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) katika uwanja wa Kijiji cha Hatwelo kata ya Ijombe Halmashauri ya wilaya ya Mbeya  leo Ijumaa Novemba 20,2020. 
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbeya , Nicodemus Tendwa akizungumza wakati wa kufunga Tamasha la sita la Jinsia Ngazi ya Wilaya lililoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) katika uwanja wa Kijiji cha Hatwelo kata ya Ijombe Halmashauri ya wilaya ya Mbeya  leo Ijumaa Novemba 20,2020. 
Afisa Mkuu wa Programu wa TGNP, Shakila Mayumana akizungumza wakati wa kufunga Tamasha la sita la Jinsia Ngazi ya Wilaya lililoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) katika uwanja wa Kijiji cha Hatwelo kata ya Ijombe Halmashauri ya wilaya ya Mbeya  leo Ijumaa Novemba 20,2020. 

Afisa Mkuu wa Programu wa TGNP ,Shakila Mayumana akizungumza wakati wa kufunga Tamasha la sita la Jinsia Ngazi ya Wilaya lililoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) katika uwanja wa Kijiji cha Hatwelo kata ya Ijombe Halmashauri ya wilaya ya Mbeya leo Ijumaa Novemba 20,2020. 
Chifu wa Kabila la Wasafwa mkoa wa Mbeya, Roketi Mwanshinga akizungumza wakati wa kufunga Tamasha la sita la Jinsia Ngazi ya Wilaya lililoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) katika uwanja wa Kijiji cha Hatwelo kata ya Ijombe Halmashauri ya wilaya ya Mbeya leo Ijumaa Novemba 20,2020. 
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mhe. Albert Chalamila akiteta jambo na Mjumbe wa Bodi ya TGNP, Jovita Mlay
Washiriki wa Tamasha la 6 la Jinsia Ngazi ya Wilaya wakicheza muziki na Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mhe. Albert Chalamila wakati wa kufunga Tamasha la sita la Jinsia Ngazi ya Wilaya lililoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) katika uwanja wa Kijiji cha Hatwelo kata ya Ijombe Halmashauri ya wilaya ya Mbeya leo Ijumaa Novemba 20,2020.
Mwanachama wa TGNP, Subira Kidiga akitoa neno la shukrani baada ya Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mhe. Albert Chalamila kufunga Tamasha la sita la Jinsia Ngazi ya Wilaya lililoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) katika uwanja wa Kijiji cha Hatwelo kata ya Ijombe Halmashauri ya wilaya ya Mbeya.
Mjumbe wa Bodi ya TGNP, Jovita akiwa na Machifu wa kabila la Wasafwa mkoa wa Mbeya.
Washiriki wa Tamasha wakicheza muziki
Meza kuu wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanajiri.
Washiriki wa tamasha wakiendelea kuburudika
Burudani inaendelea
Kushoto ni Afisa maendeleo ya jamii kutoka halmashauri ya wilaya ya Muheza, mkoani Tanga Rose Kimaro akiwasilisha mapendezo ya washiriki wa Tamasha la Jinsia kuhusu masuala ya bajeti kwa mrengo wa kijinsia ambapo alisema panahitaji ukuzaji elimu ya masuala ya bajeti kwa mrengo wa kijinsia kwa madiwani na watendaji wa halmashauri za wilaya.
Mwakilishi wa Jukwaa la Vijana Wafeminia Aisha Abdallah akiwasilisha mapendekezo kuhusu masuala ya wanawake na uongozi ambapo alisema ili kukomesha rushwa ya ngono halmashauri za wilaya zinatakiwa ziunde mikakati ya kudhibiti rushwa ya ngono kwa kushirikiana na TAKUKURU na mashirika yasiyo ya kiserikali.
Mmoja wa washiriki wa tamasha akiwasilisha mapendekezo kuhusu hali ya mazingira na mabadiliko ya tabia nchi.
Mshiriki wa Tamasha la jinsia Zawadi Kondo akiwasilisha mapendezo kuhusu mtoto wa kike,teknolojia na ubunifu ambapo alisema ili kuleta mabadiliko chanya ni lazima bidhaa ziongezwe thamani.
Washiriki wa Tamasha wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea
Wananchi wakiwa eneo la tukio
Katibu Msaidizi wa Jukwaa la Vijana Wafeminia kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Asha Nyoni akimpatia zawadi ya Tisheti Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Albert Chalamila.

Soma pia:

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post